Magufuli apokelewa kishujaa Dodoma

0

NA HAFIDH KIDO, DODOMA

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli jana alipokelewa kishujaa katika Jiji la Dodoma akitikea mkoani Manyara ikiwa ni sehemu ya ziara ya kampeni za urais kabla ya kupiga kura kesho Oktoba 28, 2020.

Akitokea wilayani Babati Mkoa wa Manyara, Dk. Magufuli alifanya mikutano kadhaa kwenye wilaya za Kondoa na Chemba kabla ya kufanya mkutano wa mwisho katika Wilaya za Chamwino na Dodoma mjini eneo la Chuo cha Mipango.

Kwa nyakati tofauti akiwa katika makaribisho jijini Dodoma, Dk. Magufuli alisimama kusalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika ikiwa ni pamoja na kuomba kura ambapo aliguswa na changamoto ya maji katika maeneo hayo hivyo kueleza katika teuzi zake za mamlaka ya maji atanzingatia viongozi wanaojiongeza tuu ‘Wanaofanya kazi nje ya box’.

“Najua hapa kuna changamoto ya maji lakini nitakapochagua waziri na wasaidizi wake wa maji nitahakilisha awe anafanya kazi Mhe ya box maana madarakani yalijengwa ili kupitisha maji kwanini maji Hamna wakati wana uwezo wa kuyavuna yakatumika kwenye shughuli mbalimbali.

“Tatizo wataalamu wanakaa na vitabu wanavyopewa nje tuu wakati mazingira ya eneo ni tofauti hivyo watendaji lazima wawe na Principal ya namna ya kutatua changamoto ya maji hususani eneo la Kondoa na Chemba tumeshindwa kitu gani wizara husika,”alisema.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally alieleza juu ya mkutano wa Dk. Magufuli na wazee wa jiji hilo pamoja na wananchi na wanachama wa CCM katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetion Center.

“Kamati zote za ushindi wanaelekezwa na Mwenyekiti na Mgombea wetu wa Urais  waendelee na kampeni bila kuchoka mpaka saa tisa alasiri kesho (leo). Saa kumi alasiri Mwenyekiti, Rais wetu na Mgombea wetu Dk. Magufuli atahutubia wanachama na wananchi wote akiwa Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, na hotuba hiyo yenye ujumbe mahususi ataitoa kupitia vyombo vyote vya habari na itakuwa mubashara,” alisema Dk. Bashiru.

Alitoa maelekezo kuwa wagombea wote wakiwemo waliopita bila kupingwa ngazi za Udiwani na Ubunge, kufanya mikutano mfululizo huku leo kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa tisa alasiri.

“Wagombea wote wakiwemo waliopita bila kupingwa ni lazima wawe wamefanya mikutano ya kuhitimisha kampeni kabla ya kuanza kumsikiliza Mgombea wa urais saa 10 alasiri,” alisisitiza.

Mkutano wa leo kwa Dk. Magufuli utakuwa ni hitimisho la safari ya miezi miwili kuzunguka nchi nzima kunadi sera za CCM ili kuwaomba wananchi ridhaa ya kuendelea na urais kwa muhula wa pili baada ya kumaliza muhula wa kwanza wa miaka mitano kwa mafanikio makubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here