Na Mwandishi Wetu
Rais Dk. John Magufuli amesema anatambua sekta binafsi ni injini ya kujenga uchumi wa kisasa na ameomba ushirikiano wa sekta hiyo katika kipindi chake cha miaka mitano.
Akizungumza katika uzinduzi wa Bunge la 12 jijini Dodoma leo Ijumaa Novemba 13, 2020, Magufuli amesema kufikia maendeleo anayoyataka serikali yake inategemea zaidi kupata mchango kutoka sekta binafsi
“Niwakaribishe wawekezaji wa ndani na nje, waje kuwekeza hapa nchini. Tanzania ni mahali sahihi pa kuwekeza. Tumebarikiwa kuwa na maeneo mengi ya kuwekeza,” amesema.
Amesema hatua kadhaa zimeendelea kuchukuliwa katika kuboresha mazingira ya biashara
“Kwa bahati nzuri tangu mwaka jana tumeanza kutekeleza mpango wa kuboresha mazingira ya biashara. Mazingira ya biashara na uwekezaji kwa miaka mitano ijayo yanatarajiwa kuwa bora zaidi,” amesisitiza kiongozi mkuu huyo wa nchi.