Maalim Seif ateuliwa Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar

0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amemteua mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo,  Maalim Seif Sharif Hamad kuwa makamu  wa kwanza wa Rais Zanzibar.

 Uteuzi huo umeanza jana Jumapili Desemba 6,  2020 na kutangazwa na katibu mkuu kiongozi wa Zanzibar,  Dk Abdulhamid Yahya Mzee.

“Kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 9(3) cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinachosomeka kwamba,   muundo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar utakuwa wa Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia.”

“Rais wa Zanzibar amemteua Maalim Seif kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, ” inaeleza taarifa hiyo.

Uteuzi huo umekuja saa chache baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati kuu ya ACT-Wazalendo kilichoridhia kushiriki katika uundwaji wa Serikali hiyo.

Baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 27 na 28,  2020 kumalizika na matokeo kutangazwa chama hicho kilidai haukuwa huru na haki na kuwazuia wanachama wake walioshinda nafasi mbalimbali kashiriki vikao  kikiwemo cha baraza la wawakilishi.

Hata hivyo, baada ya vikao na kukusanya maoni ya wanachama,  kimeridhia kushiriki kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here