Maalim Seif aapishwa kuwa Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar

0

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amemuapishwa mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar.

Hafla hiyo inafanyika leo Jumanne Desemba 8, 2020 mjini Unguja, Zanzibar na kuhudhuriwa pia na viongozi waandamizi wa ACT-Wazalendo akiwamo kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe, katibu mkuu, Ado Shaibu na naibu wake, Nassor Ahmed Mazrui pamoja na makamu mwenyekiti- Zanzibar , Juma Duni Haji.

Maalim Seif anakuwa makamu wa pili wa rais wa Zanzibar kwa mara ya pili, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2010-2016.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here