Ligi Kuu Bara kuendelea leo,  Mtibwa Sugar dhidi ya KMC

0

NA MWANDISHI WETU

LIGI Kuu Tanzania Bara msimu 2020/2021 inatarajiwa kuendelea leo kwa kuzikutanisha timu mbili za Mtibwa Sugar na KMC, Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kikosi cha KMC FC, kiliwasili mjini Morogoro jana, tayari kwa mchezo wa mzunguuko wa 15 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar. 

Ikumbukwe KMC wanakutana na Mtibwa Sugar wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi yao iliyopita dhidi Dodoma Jiji FC huku Mtibwa wakitoka sare hivyo kila upande utahiji kupata alama tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo.

Akizungumzia mchezo huo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino KMC FC Christina Mwagala, alisema wachezaji wako tayari kwa ajili ya mchezo huo.

“Kikosi chetu kimefanya maandalizi ya kutosha chini ya Makocha wazawa John Simkoko akisaidiana na Habibu Kondo na walinihakikishia kuwa vijana wana ari ya hali ya juu ya kuipigania timu yao ili kupata matokeo mazuri.

 “Tumejiandaa vizuri na tunaimani tutapambana kwenye mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar, na kupata matokeo chanya,”

“Tunawaheshimu Mtibwa Sugar, tunajua ni timu nzuri, lakini kikosi chetu hakina budi kupambana hiyo na kupata matokeo yatakayoendelea kutupa furaha.”

“Hakuna mchezo rahisi katika Ligi Kuu, lakini kwa maandalizi yaliofanywa na makocha wetu, nina imani wachezaji watapambana vizuri ndani ya dakika 90.”alisema Christina Mwagala.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu ya KMC ipo nafasi ya tano ikiwa na alama 21, huku wapinzani wao Mtibwa Sugar wakishika nafasi ya 14 na alama 16.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here