Lewandowski alivyowabwaga Messi, Ronaldo

0

NA MWANDISHI WETU

Robert Lewandowski ameshinda tuzo kubwa kabisa ya taaluma yake, na kudhihirisha kuwa mshambuliaji ambaye sio Messi au Ronaldo anaweza kupigiwa kura ya kuwa mchezaji bora wa kandanda duniani.

Nahodha huyo wa Poland ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA Mwanaume katika mwaka wa 2020 baada ya mabao yake 55 ya msimu kuisaidia Bayern Munich kunyakua mataji ya kimataifa na ya nyumbani.

Lewandowski alipata kura 52 dhidi ya 38 alizopata Lionel Messi wakati Cristiano Ronaldo akipata 35. Hafla ya tuzo hiyo ilifanyika Zurich kwa njia ya video lakini Rais wa FIFA Gianni Infantino alikwenda hadi Munich kumkabidhi binafsi Lewandowski tuzo yake. Lucy Bronze wa Uingereza alishinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.

Alishinda Ligi ya Mabingwa akiwa na Olympique Lyonnais kabla ya kuhamia Manchester City. Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alimpiku Mjerumani mwenzake Hansi Flick wa Bayern Munich na Marcelo Bielsa wa Leeds katika tuzo ya kocha bora. Manuel Neuer alishinda tuzo ya kipa bora.

Mchezaji bora Ulaya

Huu umekuwa mwaka wa mafanikio kwa Lewandowski baada ya kutwaa taji la mchezaji bora barani Ulaya kwa mwaka 2020 lililotolewa na shirikisho la Mpira wa Miguu barani Ulaya UEFA.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 32 kutoka Poland, alimpiku mchezaji mwenzake wa Bayern Manuel Neuer na kiungo wa kati wa Manchester City Kevin De Bruyne kushinda taji hilo.

Lewandowski alifunga magoli 55 katika michezo 47 msimu uliyopita wakati Bayern iliponyakuwa mataji matatu kwa kushinda Ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Ligi ya Mabingwa wa Ulaya – Champions League. Hii ndiyo mara ya kwanza kwa Lewandowski kushinda tuzo ya UEFA.

“Nashukuru sana, najivunia sana na nina furaha sana,” alisema Lewandowski. “Unapofanya kazi kwa bidii na kisha unapata zawadi hii, ni jambo maalumu sana. jivunia timu nzima kwa yale tuliyofanikisha,” aliongeza.

Kiungo wa mbele wa zamani wa Wolfsburg Pernille Harder, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Chelsea ya England, alishinda zawadi ya wanawake, huku kocha wa Lewandowski, Hansi Flick, akishinda tuzo ya kocha wa mwaka.

Lewandowski alihamia Ujerumani kutoka Poland 2010 na alikuwa sehemu muhimu ya timu ya Borussia Dortmund chini ya kocha Jürgen Klopp. Alihamia Bayern Munich 2014 akitazamia kombe la Ulaya, ambalo hatimaye liliwasili Agosti baada ya Bayern kuishinda Paris Saint-Germain 1-0 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Lewandowski alitendewa ndivyo sivyo mapema mwaka huu, wakati jarida la michezo la Ufaransa lilipotangaza kwamba halingetoa tuzo ya heshima ya Ballon d’Or msimu huu kutokana na janga la virusi vya corona.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here