Leicester City, Man U zatoka 2-2

0

ENGLAND, UINGEREZA

KIVUMBI cha Ligi Kuu England kiliendelea jana ambapo timu zinazowania nafasi ya pili Leicester City na Manchester United zilikutana na kutoshana nguvu kwa sare ya 2-2.

Mechi hiyo iliyochezwa katika Uwanja wa Kings Power unaotumiwa na klabu ya Leicester ilikuwa ya aina yake baada ya Man U kuwa inatangulia kuongoza lakini baada ya dakika chache wapinzani wao wanasawazisha.

Mechi ilianza kupamba moto baada ya mshambuliaji wa Man U Marcus Rashford kuiandikia bao la kwanza Dakika ya 23 akipokea pasi kutoka kwa Bruno Fernandes.

Lakini bao hilo lilidumu kwa dakika nane pekee kwani dakika ya 31 Harvey Barnes aliiandikia Leicester bao la kusawazisha baada ya kupokea pasi kutoka kwa James Maddison na kipindi cha kwanza kiliisha 1-1

Kipindi cha pili dakika ya 79 Bruno Fernandes alitanguliza tena Man U baada ya kuutendea haki mpira kutoka kwa Edinson Cavani lakini napo goli halikudumu kwani dakika ya 85 Axel Tuanzebe alisawazisha na hadi mpira unaisha ikawa 2-2.

Matokeo hayo yaliifanya Leicester kuendelea kubakia nafasi ya pili ikiwa na alama 28 ikiiacha Man U kwa alama moja. Hata hivyo Man U wana  mechi moja mkononi ambayo inawapa matumaini ya kuipiku Leicester andapo haitapoteza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here