LATRA yakomalia tiketi za kielekroniki

0
Mkurugenzi Mkuu LATRA (katikati), Gillard Ngewe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi, Salum Passy na kushoto Meneja Mradi wa Tiketi Mtandao LATRA, Tadei Mwita.

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kuanzia kesho Januari 6, 2020 hakuna basi litakaloruhusiwa kubeba abiria ambao hawajakata tiketi za kielekroniki katika safari ambazo imeziainisha.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe,  alisema wasafirishaji wote wa abiria kwa mabasi wanatakiwa kuzingatia masharti ya leseni za usafirishaji na matakwa ya Kanuni za Leseni za Usafirishaji – Magari ya Abiria zilizotangazwa kwa tangazo na 76 kwenye gazeti la Serikali Februari 7, 2020.

Alisema kanuni ya 4(2)© inasema leseni ya kusafirisha abiria itatolewa kwa muombaji aliyesajiliwa kwenye mfumo wa tiketi za kielektroniki ulioidhinishwa na Mamlaka.

Aliongeza kuwa Kanuni ya 24(b)(d) inamtaka msafirishaji mwenye leseni ya kusafirisha abiria wa masafa marefu ahakikishe anatoa tiketi za kielektroniki kwa abiria.

“Mamlaka inawataka wasafirishaji watoe tiketi za kielektroniki kama kanuni zinavyoelekeza. Kuanzia tarehe 6 Januari, 2021 hakuna msafirishaji atakayeruhusiwa kusafirisha abiria bila kutoa tiketi za kielekroniki kwa abiria wote,” alisema Ngewe.

Mabasi yatakayolazimika kutumia tiketi za kielekroniki ni yanayofanya safari zake kati ya Dar-es-Salaam na Tanga, Tunduma, Rukwa, Lindi, Morogoro, Mtwara, Kilombero, Iringa, Ifakara, Malinyi, Njombe, Ruvuma, Mahenge, Mbeya na yale ya Tanga-Arusha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here