Kocha Barcelona, awashambulia wachezaji wake kwa uzembe

0

MADRID, HISPANIA

KOCHA wa miamba wa Uhispania Barcelona Ronald Koeman amewashambulia wachezaji wake kwa kukubali goli kwa urahisi walipofungwa 2-1 na Cadiz wiki iliyopita katika mechi ya Ligi Kuu ya Uhispania La Liga.

Alvaro Negredo ndiye aliewafungia Cadiz hilo goli la ushindi baada ya makosa kadhaa yaliyofanywa na wachezaji wa Barcelona.

Koeman, alisema yote hayo yametokea kwasababu wachezaji wake hawakuwa makini.

“Kwa kweli nafikiri ni hatua iliyoturejesha nyuma sana katika harakati zetu za kutaka kujaribu tulishinde taji. Lazima tuitazame tena mechi hii ambayo matokeo ya mwisho yanavunja moyo sana na ni lazima tukubali na tujaribu kuwa bora zaidi.

Tuko pointi 12 nyuma ya Atletico Madrid ambayo kwa sasa ni timu nzuri sana, na pointi hizo ni nyingi ila lazima tuendelee kufanya bidii.

Bado tuna mechi kadhaa za kucheza ila ni kweli kwamba tusipojitahidi na kuuboresha mtazamo wetu wa mechi, basi kama timu hatutaimarika.

“Tunastahili kupata matokeo nyumbani na ugenini,” alisema Koeman.

Kwa sasa Barcelona wanaishikilia nafasi ya tisa katika msimamo wa La Liga huku Atletico Madrid wakiongoza na alama 26 huku Real Sociedad wako alama moja nyuma yao katika nafasi ya pili na Villareal ni watatu wakiwa na pointi 21 na mabingwa watetezi Real Madrid ni wanne wakiwa na pointi 20.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here