Kizimbani kwa kumlawiti mtoto wa miaka 9

0

NA DEVOTHA FULUGUNGE, DAR ES SALAAM

KIJANA mmoja amefikishwa katika Mahakama ya  Mkazi kinondoni kujibu shtaka moja la kumuingilia kinyume na maumbile mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 9.

Mshtakiwa huyo Vicent George (19) ambaye ni Mkazi wa Kibaha, alifikishwa Mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Ester Mwakalinga .

Akisoma shtaka hilo, Wakili wa Serikali Hilda Katto, alidai mshtakiwa George anadaiwa kuwa kati ya tarehe zisizojulikana za mwezi Mei, 2019 maeneo ya Mbezi Luis uko Ubungo jijini Dar-es-Salaam mshtakiwa alimuingiza mtoto wa miaka 9 (jina limehifadhiwa) uume wake sehemu ya haja kubwa.

Hata hivyo, mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo upande wa Wakili Katto alisema upelelezi umekamilika.

Pia, Kwa upande wa Hakimu alisema dhamana ipo wazi ambapo mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili mmoja awe ni mtumishi wa Serikali na kusaini bondi ya Sh. milioni 2.

Mshtakiwa hakufanikiwa kukidhi vigezo vya dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here