Kizimbani kwa kijipatia Sh. Mil 100 baada ya kujifanya Afisa Usalama

0

NA DEVOTHA FULUGUNGE, MUM

Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imempandisha kizimbani Patrick Hamphrey mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Mwenge kwa makossa mawili likiwemo kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh. milioni 100 na kujitambulisha kama Afisa Usalama.

Mashitaka hayo yalisomwa jana na wakili Neema Mushi katika mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Luboroga na kudai kuwa  mnamo Agosti 17, 2020 mtuhumiwa alijifanya afisa usalama kwa kujitambulisha kama Frank Peter Kimoso na kujipatia kiasi hicho cha fedha.

Wakili Mushi aliendelea kudai kuwa fedha hizo zilitoka kwa Isaya Costa Sanga ambaye alikwepa kulipa kodi ya serikali hivyo aliahidiwa kusaidiwa endapo angelipa fedha hizo.

Hata hivyo baada ya kusomwa kwa mashtaka hayo mtuhumiwa alikana kwa kudai  taarifa hizo hazikuwa na ukweli ndani yake.

Hakimu Luboroga alisema dhamna ipo wazi ambapo mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamani wawili na kuweka bondi ya kiasi cha Sh. milioni 50 au hati ya nyumba yenye thamani hiyo.

Mshtakiwa hakuweza kutimiza masharti yaliyotajwa na hakimu hivyo kupelekwa rumande ambapo kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 3, 2020.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here