Kiongozi Palestina atibiwa Israel

0

TEL AVIV, Israel

OFISA wa juu wa Palestina, Saed Erekat yuko kwenye uangalizi maalumu baada ya kuugua maambukizi ya ugonjwa wa corona na amelazwa katika hospitali nchini Israel, imeelezwa.

Taarifa iliyotolewa jana ilisema kiongozi huyo wa juu wa Palestina, amelazwa Israel toka juzi katika hospitali ya Hadassah iliopo mjini Yerusalemu, ambapo alichukuliwa kutoka nyumbani kwake Yeriko, katika eneo la Ukingo wa Magharibi.

Ilisema hali ya kiongozi huyo sio nzuri na amekuwa mahututi wakati alipokuwa akipatiwa oksijeni na hali yake ilikuwa inabadilika mara kwa mara na kushindwa kupumua na aliwekwa kwenye mashine ya msaada wa kupumua.

Pia, ilisema kumtibu Erekat ilikuwa changamoto kubwa kwa kuwa aliwahi kufanyiwa upasuaji kupandikiza mbavu miaka mitatu iliyopita, na alikuwa na mfumo wa kinga ulio dhaifu na maambukizi ya vijidudu mbali na kuwa na virusi vya corona.

Erekat ni Katibu Mkuu wa chama cha Palestine Liberation Organisation (PLO), akihudumu kama mshauri wa Rais Mahmoud Abbas na amekuwa mpatanishi mkuu wa mazungumzo ya amani ya Palestina na Israel kwa kipindi cha miongo miwili na nusu.

Alijitangaza kuwa na maambukizi ya corona, katika ukurasa wake wa twitter kuwa ana dalili kali kutokana na kushuka kwa kinga kutokana na kupandikizwa mbavu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here