Kingu atetea kiti chake Singida Magharibi

0

Elibariki Kingu wa CCM, ametetea kiti chake cha ubunge jimbo la Singida Magharibi kwa kupata kura 32,720 kati ya kura 41,068.

Akitangaza matokeo ya jimbo la Singida Magharibi msimamzi wa uchaguzi Justice Kijaji amemtangaza Kingu kuwa ameshinda ubunge, huku Hemed Ramadhan wa Chadema amepata kura 7,446 na Sufiani Juma wa ACT-Wazalendo kura 902.

Kijazi amesema waliojiandikisha katika jimbo hilo ni 90,980, waliopiga kura walikuwa 41,068 huku kura 1435 zikikataliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here