Kikundi cha Chapakazi kinavyopambana kuifanya Dodoma ya kijani

0

Na Dotto Kwilasa, Dodoma

KUTOKANA na Serikali ya awamu ya tano kuhamasisha jamii kuhusu namna ya kujanikisha mkoa wa Dodoma ili uwe na hadhi ya makao Makuu ya nchi, kikundi cha kutunza na kuhifadhi mazingira cha ‘Chapakazi’ kimetoa wito kwa jamii kutumia mvua zinazoendelea kunyesha nchini kupanda miti ya matunda na vivuli ili kulinda na kutunza mazingira.

kinajishughulisha na uuzaji wa miche ya matunda na vivuli kinapatikana katika eneo la barabara ya Iringa mkoani Dodoma.

Akizungumza Katika mahojiano maalumu na Jamvi online leo, Disemba 23 mwaka huu Jijini Dodoma, Mtunza fedha wa kikundi hicho Darwesh Said amesema ili kuifanya Dodoma kuwa ya kijani sharti kutumia mvua za mwanzoni kupanda Miche inayoendana na hali ya hewa ya mkoa wa Dodoma.

“Unapofanya maamuzi ya kupanda miche lazima upate ushauri wa ,miti mingi inategemea zaidi Hali ya hewa ya sehemu husika,

Hapa kwetu kuna miche ya kila aina na tumekuwa tukiwapandia watu garden sasa huu ndio wakati wa kupanda miche ya kila aina ili iweze kuota vizuri lakini pia na kutunza mazingira,”amesema Darwesh.

Amesema katika kikundi chao,miche ya matunda inayopatikana ni pamoja na Miembe, Michungwa, Miparachichi na Milimao ambayo yote inastahimili hali ya hewa ya mikoa ya Kanda ya Kati.

Ameitaja miche mingine iliyopo ni pamoja na Miche ya kimvuli,ambayo ni Mitimaji,Miarobaini, Mitingia na Codian, Miche mingine iliyopo ni ya mbao ambayo ni Greveria, Mitiki,

Kwa upande wa maua amesema yaliyopo ni Biscas, Exola, Jesus, Lamanda pamoja na Maua aina ya Parma ambayo ni Royal Palm, Travell Parm na Golden Parm.

Darwesh pia amesema katika eneo lao hilo kunapatikana vyungu vya kila aina vikiwemo vinavyotengenezwa kwa vigae.

“Pia katika eneo hili watu wanapiga picha kwa ajili ya kumbukumbu pamoja na maharusi lakini tumekuwa tukitembelewa na wadau mbalimbali,” amesema.

Mtunza fedha wa Kikundi cha Chapakazi Darwesh Said akionesha baadhi ya vyungu vya kupandia maua walivyo navyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here