Kiduku: Hadi sasa sijalipwa fedha zangu za pambano la Sirimongkhon

0

NA MWANDISHI WETU

BONDIA Mtanzania Twaha Kiduku amesema kuwa hadi sasa hajalipwa fedha zake zilizobaki katika malipo ya pambano lake dhidi ya Mthailand Sirimongkhon Lamdhwan.

Ikumbukwe pambano hilo la uzito wa Kati lilifanyika Oktoba 30, 2020 kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam.

“Mpaka sasa sijalipwa fedha zangu zilizobaki ambazo ni nyingi mno ukilinganisha na kiasi kidogo nilicho chukua kama utangulizi katika pambano langu dhidi ya Mthailand Sirimongkhon kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba ambapo nilishinda kwa TKO usiku huo wa Vitasa,”alisema Kiduku.

Twaha Kiduku, aliyasema hayo baada ya kuandika ujumbe ambao unawatetea Mabondia wenzake waliyokosa nauli ya kurejea kwao Simbawanga pamoja na hela ya kula wakiwa Dodoma baada ya kukimbiwa na Promota licha ya kuandikishiana mikataba.

”Pambano langu na Mthailand sijalipwa pesa zangu, nilipata robo tu ya pes zote, Promota Shomari Kimbau.

Viongozi wa mchezo wa Ngumi wapo kimya tu, sijui wanachoshindwa ni nini ?, naiomba serikali iingize mkono wake, pambano langu sijalipwa hela na wala mpaka leo halijaingizwa kwenye rekodi  ?”

Twaha Kiduku alishinda pambano hilo kwa TKO dhidi ya Mthailand Sirimongkhon raundi ya 7, pambano la uzito wa kati lililopigwa Oktoba 30, 2020 kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba.

Hata hivyo, kuna taarifa kuwa, Kimbau amefungiwa kujihusisha na mchezo huo kwa muda wa mwaka mmoja huku akipigwa faini ya Sh. Mil. 1, kutokana kitendo hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here