Kenyatta afuta uwezekano wa Marekani kushambulia al-Shabab kutoka Kenya

0

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekiambia kituo cha habari cha France 24 kwamba hataidhinisha mashambulizi ya kutumia ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab katika ardhi ya Kenya.

Rais Kenyatta ambaye yuko nchini Ufaransa kwa ziara rasmi ya kikazi amesema hajapokea ombi lolote kama hilo.

Mwezi uliyopita gazeti la New York Times lilinukuu vyanzo vya serikali ya Marekani ikisema majeshi ya nchi hiyo yanatafuta idhini ya kushambulia ngome za al-Shabab kutoka mashariki mwa Kenya.

Ripoti hiyo ilitolewa siku kadhaa kabla ya mahakama ya kijeshi nchini Somalia kumhukumu mwanamgambo mmoja wa Kislam kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusika na shambulio dhidi ya kambi ya jeshi la Marekani nchini Kenya.

Shambulio hilo lilikuwa la kwanza kutekelezwa na wanamgambo wa al-Shabab dhidi ya vikosi vya Marekani nchini Kenya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here