Kauli ya Magufuli baada ya kupiga kura

0

Na Mwandishi Wetu

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli amepiga kura wilayani Chamwino mkoani Dodoma na kuwataka Watanzania kudumisha amani.

Akizungumza baada ya kupiga kura leo Jumatano Oktoba 28, 2020, Magufuli aliyeongozana na mkewe, Janeth amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

“Watu wamejitokeza kwa wingi, kwa hiyo nawapongeza kwa usimamizi mzuri ambao uko hapa. Wito wangu kwa Watanzania tujitokeze kwa wingi kupiga kura, twende tukapige kura ambayo kila mmoja atakuwa nayo katika moyo wake.”

“Nipende kusisitiza, amani lazima tuendelee kuitunze kama Taifa kwa sababu kuna maisha hata baada ya uchaguzi. Mungu awabariki wapiga kura wote Mungu aibariki Tanzania, Asanteni sana Watanzania.

“Mimi nimeshapiga kura na mke wangu ameshapiga kura kwa hiyo tumetimiza wajibu wetu wa kuchagua,” amesema Magufuli.

Rais Dk. John Magufuli na mkewe Janeth Magufuli wakiwasili katika Kituo cha Kupigia Kura cha Idara ya Maji Chamwino Ikulu kwa ajili ya kupiga Kura leo Oktoba 28, 2020.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here