Kasongo: Kuwa na viwanja bora inawezekana

0

NA RESTUTA KAYOMBO, TUDARCO

UONGOZI wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TBPL), umeweka wazi kwamba inawezekana kabisa kuwa na viwanja bora endapo tu wadau wa Soka watasimamia utaratibu, kanuni na sheria zinazoendesha mchezo wa mpira walizojiwekea.

Hivi karibuni TBPL ilivifungia baadhi ya viwanja baada ya kubainika kuwa vimeshindwa kukidhi vigezo vinavyotakiwa katika mchezo wa mpira.

Mtendaji Mkuu wa TBPL, Alimas Kasongo, aliyasema hayo, wakati alipotoa taarifa za maendeleo ya viwanja vilivyokuwa vimefungwa kutokana na kasoro zilipoteza ubora.
“Utaona kwamba sio jambo la masihara ni jambo ambalo tumedhamiria kwamba tuweze kutoka hapa tulipo tuweze kufika pale ambapo kila mmoja wetu anatamani.

“Unaweza ukaona viwanja vilivyokuwa vimefungwa vinarudi… Kimerudi kiwanja cha Gwambina kikiwa katika ubora wake, kimerudi kiwanja kile cha Biashara pale Karume Mara kikiwa kwenye ubora wake.

“Unaweza ukaona leo Jamhuri imerudi ikiwa kwenye ubora wake kabisa kila mmoja anatamani iwe hiyvo, unaweza ukaona Ushirika bado tunaendelea kuusimamisha, mpaka pale tutakapo jiridhisha kama uko tayari,”alisema Kasongo.

Kasongo, alisema bado pia kiwanja cha Mabatini mkoani Pwani bado kinaendelea kufungwa hadi pale kitakapo kuwa tayari ndiyo kitaruhusiwa kutumika.

Alisema, bado wanaendelea kuvifuatilia viwanja vingine na wakibaini vimepoteza ubora lakini pia havikidhi matakwa ya kikanuni na Sheria namba moja basi navyo vitafungwa.
“Kwa kweli kuwa na viwanja bora inawezekana kabisa, sisi sote ni mashuhuda, tumeshuhudia na hivi vitu vinaweezekana kabisa wala sio ndoto, wala sio vitu vya kuigiza.

“Ni vitu ambavyo kama tutasimamia utaratibu, kama tutasimamia kanuni zetu tulizojiwekea mimi naamini inawezekana lakini pia nishukue nafasi hii kuwapongeza wadau wa soka kwani mara baada yakuifanya agendana kuizungumza na kuisamba i
mesaidia.

“Kwani baada ya kuizungumza sana nayo ikawafanya wakuu wa mikoa, ikafanya wadau wa pale mikoani imewafanya waanze kushirikiana kwa kuona ni jinsi gani ambavyo tunaweza kuukosa mpira ni jambo ambalo haliwezekani etu kwa sababu tuna  kwa sababu tu tuna kiwanja ambacho hakikidhi sifa za kikanuni na sheria namba moja.

“Kwa hiyo mkoa uwanja wake unapofungiwa wanalichukua kuwa ni agenda ya mkoa utaanza kuona serikali ya mkoa, utaona wadau wote wanahangaika, huyu kaleta maji huyu kaleta hiki ili mradi wanahakikisha kiwanja kinakuwa kwenye mazingira amabayo yanatakiwa kwa mujibu wa sheria,”alisema Kasongo.

Kasongo, alisema kuwa na usimamizi na kuwa na viwanja bora jambo hilo linawezekana tena zaidi hivyo vilivyofanywa huku akisisitiza kwa wadau wa michezo kuendeleza mjadala wa kuzungumzia viwanja na mambo yote ambayo hayapendezi kwenye mpira na mwisho wa siku yabaki kuwa historia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here