Kampuni ya New Habari yasitisha uzalishaji magazeti

0

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya New Habari 2006 LTD inayozalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa na Dimba imetangaza kusitisha uzalishaji kutokana na mwenendo mbaya wa biashara.

Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo leo Ijumaa Desemba  3, 2020 jijini Dar es Salaam, mhariri mtendaji, Dennis Msacky amesema uzalishaji wa magazeti hayo utasitishwa kuanzia Jumatatu Desemba 7, 2020.

“Ni kweli tumesitisha biashara kutokana na mwenendo mbaya wa biashara. Kuanzia Jumatatu na kuendelea hatutakuwa na uzalishaji kabisa,” amesema Msacky.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here