Kamati ya uongozi ACT yateua jina la Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar

0

Na Mwandishi Wetu

Baada ya Chama cha ACT Wazalendo kuridhia kushiriki kwenye  Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar  (SUK), tayari kamati ya uongozi imewasilisha serikalini jina la atakayekuwa makamu wa kwanza wa rais.

Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya tafakuri ya kina iliyofanywa na kamati kuu iliyokutana jana jijini Dar es Salaam.

Amesema baada ya kutafakari kwa kina pamoja na mawazo ya wanachama, wameridhia kushiriki kwenye serikali hiyo kwa mustakabali mpana wa Zanzibar.

Ado ameyasema hayo leo Jumapili Desemba 06, 2020 alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

Sambamba na kupelekea jina hilo, Ado amesema kamati kuu imewaruhusu wawakilishi, wabunge na madiwani  waliochaguliwa kupitia chama hicho kuendelea na majukumu waliyopata.

“Chama kimefikia uamuzi huu sio kwa kupenda au tumefurahia hakuna asiyefahamu kwamba uchaguzi ulivurugwa na kuharibiwa lakini hii ni njia nafuu ya kuendeleza mapambano.

Tunataka serikali hii iendelee kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizojitokeza kwenye uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote walishiriki kuvunja haki za binadamu,” amesema Shaibu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here