Kaduguda agoma kusema kama atagombea au hata gombea

0

NA MWANDISHI WETU

BAADA ya uongozi wa Simba SC kutangaza kuanza mchakato wa Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti, Kaimu Mwenyekiti wa timu hiyo, Mwina Kaduguda ameweka wazi kuwa kabla ya kuingia kwenye hatua hiyo, alitarajia baadhi ya mambo yangefanyika kwaza.

Ikumbukwe nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu aliyekuwa mwenyekiti klabu ya Simba, Swedi Mkwabi kuamua kujiuzulu nafasi hiyo kwa kile alichodai kuwa anahitaji muda zaidi ili kusimamia shughuli zake binafsi.

Mwaka jana Septemba 14, 2019 na uongozi wa klabu hiyo ya Simba iliwajulisha wanachama, mashabiki na wananchi wote, kujiuzulu Mkwabi.

Swedi aliamua kuiandikia barua Bodi ya Wakurugenzi kupitia Mwenyekiti wa Bodi akitoa taarifa hiyo ya kujiuzulu kwake.

Jana, akifanyiwa mahojiano kwenye kipindi cha Sports Arena kinachorushwa na Wasfi FM, Kaduguda alishindwa kuweka wazi kuhusu kama atagombea au la.

“Kwenye Bodi ya Wakurugezi wa Simba wote wanakubaliana kuhusu maendeleo ya timu lakini kuna kitu (hata hivyo alikuwa mgumu kukitaja kitu hicho), alisema Kaduguda ambaye kwa sasa anakaimu nafasi hiyo kwa zaidi ya mwaka sasa.

Licha ya kutokuwa muwazi lakini ni wazi kwa kauli yake inaonesha kwa upande wake kuna kitu hakijakwenda sawa hivyo akitamani kifanyike kwanza.

Aidha, Kaduga alikataa kabisa kuweka wazi kama atakuwa ni miongoni mwa wanachama watakaoingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Desemba 12, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara klabu ya Simba, ilitangaza mchakato mzima wa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti ambao ulianza Desemba 13, huku ukitarajiwa kukamilika Februari 7, mwakani,

Ikumbukwe nafasi hiyo kwa sasa inshikiliwa, kwa muda na Mwina Kaduguda baada ya kuachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Swedi Mkwabi aliyejiuzulu wadhifa huo Septemba 14, mwaka jana baada ya kuhudumu kwa takribani miezi 10 pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ndani ya klabu hiyo, Boniface Lihamwike alisema: “Tunataka kuwahakikishia Wanasimba na wadau wote wa michezo kiujumla kuwa uchaguzi huu utakuwa huru na wa haki,”

Akitoa ratiba ya mchakato huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Steven Ally alisema: “Mchakato wa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Simba umeanza rasmi baada ya taarifa hiyo, na utaendelea mpaka Februari 7, mwaka 2021 ambapo ndiyo tunatarajia kufanya uchaguzi na kutangaza mshindi wa nafasi hiyo,”

“Kwa taarifa zaidi kuhusu mchakato mzima tumebandika ratiba hii makao makuu ya klabu lakini pia watu wanaweza kuipata kupitia mitandao yetu ya kijamii, vigezo vya kuchukua fomu ni vile ambavyo vimewekwa bayana na Ibara ya 27 ya katiba ya klabu na pia vinapatikana kwenye fomu.

“Lakini kwa uchache ni lazima mgombea awe na elimu ya angalau Shahada inayotambuliwa na tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU), na kadi ya mwanachama hai kwa miaka mitatu huku gharama kwa fomu ikiwa ni Sh. 300,000 (laki tatu)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here