Jurgen Klopp alia na VAR

0

LONDON, UINGEREZA

JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa mashine ya kujiridhishia na maamuzi ndani ya uwanja maarufu kama VAR ilitoa penalti isiyo sahihi kwa Sheffield United.

Liverpool ikiwa Uwanja wa Anfield ilishinda mabao 2-1 ambapo Sheffield United ilianza kufunga kwa penalti dakika ya 13 kupitia kwa Sander Berge.

Bao hilo lilisawazishwa dakika ya 41 na Roberto Firmino na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu na Diogo Jota alipachika bao la ushindi kwa Liverpool dakika ya 64.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Uingereza walianza bila ya uwepo wa nyota wao Virgil van Dijk ambaye anaweza kukaa nje msimu mzima jambo linalowafanya Liverpool kufikiria kuongeza beki mwingine Januari.

Klopp alisema kuwa maamuzi mengine hayakuwa sahihi kwenye mchezo huo ikiwa ni pamoja na penalti jambo ambalo linawapa maumivu.

Penalti hiyo ilipatikana baada ya Fabinho kumchezea faulo Oil McBurnie karibu na eneo la 18 na VAR iliamua iwe penalti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here