Jumba la kumbukumbu la Pele kufunguliwa Brazil

0

BRASILIA, BRAZIL

MRADI mkubwa wa kumkumbuka gwiji wa zamani wa soka Pele wametekelezwa nchini Brazil baada ya shughuli za miezi miwili na siku 45.

Mashabiki wa Santos hawamkusahau gwiji wa soka Pele anayekaribia kufikisha miaka 80 katika siku ya sherehe ya kuzaliwa kwake.

Katika mradi huo wa kuifufua Santos, sehemu nyingi za mji kama vile migahawa, bandari na treni zilipambwa kwa michoro ya Pele.

Msanii Eduardo Kobra aliyehusika na michoro hiyo pia alipewa pongezi nyingi kutoka kwa wakaazi wenzie wa mji.

Kwa upande mwingine, jumba la kumbukumbu la Pele lililokuwa limefungwa nchini Brazil tangu mwezi Machi kutokana na janga la corona, pia lilifunguliwa.

Pele ataingia miaka 80 siku ya tarehe 23 Oktoba.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa jumba la kumbukumbu, maonyesho hayo yanalenga kumtambulisha Pele kama mchezaji bora wa zamani, kwa mashabiki wapya wa kizazi hiki cha Ronaldo na Messi.

Jumba la kumbukumbu la Pele litafunguliwa kwa watalii na kuachwa wazi hadi mwezi Aprili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here