Jumba la kifahari la  Michael Jackson lauzwa  kwa hasara

0

NEWYORK,MAREKANI

RAFIKI WA zamani wa  mwanamuziki nguli duniani  hayati  Michael Jackson Ron Burkle, hivi majuzi alinunua nyumba iliopo katika shamba hilo huko Los Olivos, California, msemaji wake alisema .

Alilipa $22m (£16.2m) kwa jumba hilo la kifahari, limesema jarida la Wall Street Journal, akiweka wazi rekodi zake na kuwataja watu watatu waliohusika katika makubaliano hayo.

Jumbe hilo lililojengwa katika ekari 2,700 (1,100 hectare) kwa mara ya kwanza lilinadiwa kwa $100m  mwaka   2015.

Tangu wakati huo jumba hilo la Neverland, lililopo kaskazini mwa mji wa Santa Barbara limekuwa likiuzwa hivi karibuni kwa $31m.

Jackson alinunua jumba hilo kwa $19m, ambalo baadaye alililitaja baada ya kisiwa kisichojulikana katika kitabu kilichoandikwa na Peter Pan .

Mwanamuziki huyo alilinunua jumba hilo mwaka 1987 , na kulifanya kuwa nyumbani kwake wakati wa umaarufu wake..

Alibadilisha jumba hilo na kuwa eneo  la burudani , akijenga eneo la kufuga wanyama mbali na ukumbi wa chini ya ardhi ambapo aliwafurahisha watoto na familia zao.

Miaka 1990 na 2000 , Jumba hilo lilichunguzwa sana kutokana na madai ya udhalilishaji watoto kingono dhidi ya msanii huyo.

Jackson alikana madai hayo yaliowasilishwa na kiongozi wa mashtaka wa eneo la Santa Barbara kwamba alitumia jumbe hilo kuwakuza watoto.

Mwaka 2005, Jackson alishtakiwa na kuachiliwa huru kwa madai kwamba alimnyanyasa mvulana wa miaka 13 katika jumbe la Neverland.

Jackson hakurudi tena katika jumba hilo na miaka minne baadaye mwezi Juni 2009, Jackson alifariki katika nyumba yake nyengine mjini Los Angeles baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo uliotokana na kula dawa kupitia kiasi.

Tangu kifo chake Jackson amekuwa akikumbwa na madai ya unyanyasaji ikiwemo yale yaliochapishwa katika makala moja kwa jina kuondoka Neverland 2019.

Jumba la Neverland limebadilishwa jina na kuitwa Sycamore Valley Ranch na limefanyiwa ukarabati mkubwa tangu kufariki kwa msanii huyo .

Msemaji wa Burkle alisema kwamba mfanyabiashara huyo alitumia fursa ya ardhi iliopo katika jumba hilo kununua jumba hilo.

Aliiona nyumba hiyo kutoka angani alipokuwa akitafuta ardhi na mara moja akawasiliana na Tom Barrack , mwanzilishi wa kampuni ya LLC ili kununua jumba hilo.

Bwana Burkle mwenye umri wa miaka 68 , ni mwanzilishi na msimamizi mwenza wa Yucaipa Companies, LLC, kampuni ya uwekezaji wa kibinafsi .

Thamani ya Burkle kufikia tarehe 24 mwezi Disemba 2020 ilikuwa $1.4bn, kulingana na jarida la Forbes.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here