Jina la mrithi wa Maalim Seif tayari lapendekezwa

0

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema tayari wameshapendekeza jina la atakayemrithi aliyekuwa Makamu wa Rais wa kwanza Zanzibar na Mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki dunia tarehe 17 mwezi huu.

Akizungumza kwenye Khitma ya kumuombea Maalim Seif  iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, amesema Marehemu Maalim Seif aliacha maelekezo juu ya nini kifanyike endapo ikitokea akatangulia mbele ya haki.

“Tayari tumeshapendekeza jina kwa Rais wa Zanzibar la mtu ambaye atarithi majukumu ambayo Maalim Seif alikuwa anayafanya, bahati nzuri, Maalim alikuwa ni kiongozi alijua kuna siku Mwenyezi Mungu atamchukua kwa sababu sisi sote lazima turejee kwa Mwenyezi Mungu kama tulivyoambiwa na mafunzo ya dini yetu na dini zote,” amesema Zitto Kabwe.

Aidha, Zitto amesema chama kinaamini katika huyo waliyempendekeza ataweza kusimamia maridhianao na haki za Wanzazibari huku akiomba wananchi waendelee kuwaombea dua katika kupigani demokrasia na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani.

“Sisi tunaamini kabisa kuwa huyo ambaye amependekezwa ataweza kusimamia maridhiano na haki za Wazanzibari kama ambavyo Maalim Seif mwenyewe alikuwa akifanya,” amesema Zitto Kabwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here