Jibu la Magufuli kwa wanaosema hampendi Gambo

0
Mgombea Urais kupitia CCM, Rais Dk. John Magufuli akizungumza na Wananchi wa Arusha katika mkutano wa Kampeni za Urais uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Oktoba 23, 2020

Na Mwandishi Wetu

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli ameeleza kushangazwa kwake na watu wanaomsema kuwa hampendi mgombea ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya chama hicho, Mrisho Gambo.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha leo Ijumaa Oktoba 23, 2020, Magufuli amesema Gambo ndio atakayekwenda kuikomboa Arusha.

Magufuli amesema alipata wakati mgumu kupeleka maendeleo Arusha kutokana mji huo kuongozwa na upinzani hivyo alimpeleka Gambo kwenda kufanya mabadiliko.

“Nilipata wakati mgumu sana Arusha hadi nikaamua kumteua Gambo ili awe ananipa taarifa za hapa. Nilimwambia Gambo nenda kafanye kazi kama mkuu wa mkoa na mbunge wa Arusha mjini na amefanya kazi nzuri mno.”

“Sikumfukuza ukuu wa mkoa wala aliyekuwa mkuu wa wilaya wa hapa. Gambo aliniomba kwa kuniambia kuwa ameiona Arusha inakwenda vibaya ninaomba nikaikomboe nikamwambia nenda na Mungu akusaidie.

”Ninawashangaa watu wanaposimama kwenye majukwaa na kusema Gambo simpendi, ningekuwa simpendi ningerudisha jina lake aje kugombea?” amehoji Magufuli.

“Gambo sikumfukuza kuwa RC, kama ilivyokuwa kwa wengine kwani tulitenda haki kwamba Ma-RC, DC, DAS wote waliokwenda kugombea Ubunge tulitengua uteuzi wao na ndicho nilichofanya kwa Gambo, na bahati nzuri aliniomba. Hata DC wa hapa alienda kugombea wala sikumtengua.

“Ninawashangaa watu wanaposimama kwenye majukwaa wanasema Gambo simpendi, ningekuwa simpendi ningemrudisha jina lake kuja kugombea? Wana Arusha kama mnataka maendeleo ya kweli nileteeni Gambo aje ‘agambulile’ maisha ya maendeleo ya kweli” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here