Jamvi la Habari mabingwa TFF Media Bonanza 2020

0

Na Bethsheba Wambura, Dar es Salaam 

JAMVI LA HABARI imeibuka mshindi  na kunyakua kombe baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 7-6 dhidi ya Global Publishers katika mchezo wa TFF Media Day Bonanza uliochezwa leo Disemba 06, 2020 Uwanja wa Leaders Club Kinondoni. Awali timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Kabla ya kufika fainali JAMVI LA HABARI ilicheza mechi mbili za kwanza dhidi ya Mwananchi Communications Ltd na kuwatoa kwa mikwaju ya penati 7-6 na kuingia nusu fainali dhidi ya Uhuru Publications na kufanikiwa kufuzu fainali kuingia fainali na Global Publishers.

Akizungumza mmoja wa wachezaji wa Timu ya Jamvi, Said Malinda amesema mchezo huo haukuwa rahisi lakini walijipanga kuhakikisha wanashinda.

Baada ya kushinda wachezaji na kipa wa JAMVI LA HABARI walitunukiwa medali na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia.

“Mchezo ulikuwa mgumu na Timu zote zilijiandaa Ila sisi tulikuja tukijua kabisa tutashinda, maandalizi ya Bonanza yalikuwa mazuri japo suala la muda na maamuzi ya marefu yalileta utata kidogo ila kila kitu kimeenda vizuri na tunafurahia ushindi wetu,” amesema Malinda.

Tamasha la Media Bonanza Day hufanyika kila mwaka na huandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kudhaminiwa na Kampuni mbalimbali ambapo kwa mwaka huu limedhaminiwa na Benki ya KCB.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here