Home Uncategorized Jaji Mutungi awataka viongozi wa Vyama vya siasa kutoa elimu ya Corona

Jaji Mutungi awataka viongozi wa Vyama vya siasa kutoa elimu ya Corona

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam


Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuweka itikadi zao pembeni na badala yake watumie ushawishi kutoa elimu na kuwaleta Watanzania pamoja ili waweze kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya corona.

Jaji Mutungi amebainisha bila kufanya hivyo ugonjwa huo utaendelea kusambaa na athari zake zitaonekana kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Taarifa ya Jaji Mutungi aliyoitoa jana Alhamisi Machi 19, 2020 alisema vyama vyote na wadau wa siasa wanapaswa kuunga mkono jitihada na miongozo iliyotolewa na Serikali ili kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo ambao umeingia nchini humo.

Tayari watu sita wameripotiwa kuwa na corona huku Serikali ya Tanzania ikiwataka wananchi kuchukua tahadhari ikiwamo kuzuia mikusanyiko ya watu. 

“Nitumie fursa hii kuvisihi vyama vya siasa viendelee kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wanachama na wafuasi wenu wanatekeleza kwa vitendo maelekezo yaliyokwisha tolewa,m kwa manufaa ya taifa letu kwa ujumla,” alisema.

Jaji Mutungi aliongeza; “ nikiwa kama mlezi wa vyama vya siasa natoa rai kwa viongozi wa vyama vya vyote vya siasa nchini na wadau wote wa siasa kuunga mkono jitihada na miongozo inayotolewa na Serikali kupambana na maambukizi ya ugomjwa huu hatari ambao umeikumba dunia. 

“Ugonjwa huu ni hatari kama wataalamu wanavyoelimisha na athari zake ni pana, hivyo kama taifa tunatakiwa kushikamana katika kukabiliana na maambukizi yake.” 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular

Yanga yampatia Tshishimbi mkataba mpya

NA MWANDISHI WETU Klabu ya Yanga SC, imesema kuwa tayari imemaliza kazi yake ya kuhakikisha inambakiza kiungo tegemeo wa...

Tetesi za soka barani Ulaya

SANCHO AITIKISA UNITED Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jadon Sancho (20), amesema hatakuwa tayari...

Makonda: Wazururaji hawatakwenda mahabusu watazibua mitaro ya maji machafu

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa watu watakaokamatwa kwenye mkoa huo kutokana...

Chui katika hifadhi ya wanyama ya Bronx akutwa na Virusi vya Corona

NEW YORK, MAREKANI Chui wa kike wa Malaysia aliyefahamika kwa jina la Nadia mwenye umri wa miaka minne katika hifadhi...

Recent Comments