Israel kufanya uchaguzi wa nne ndani ya miaka miwili

0

JERUSALEMU, ISRAEL

ISRAEL itafanya uchaguzi wake wa nne katika kipindi cha miaka miwili baada ya vyama vikuu viwili katika serikali ya umoja kushindwa kuheshimu muda wa mwisho wa kutatua mzozo juu ya bajeti ya taifa.

Wapigakura watarejea katika uchaguzi mwezi Machi, miezi 12 tu baada ya awamu ya uchaguzi kufanyika.

Uchaguzi wa awali haukukamilika , na hivyo kusababisha kuundwa kwa serikali nadra ya umoja.

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu, ambaye kesi ya madai ya ufisadi inaendelea dhidi yake, ana matumaini ya kurejea madarakani kwa muhula wa sita.

Alikana mashitaka ya uhalifu, ambayo aliyapuuzilia mbali akiyataka kuwa yenye uchochezi wa kisiasa.

Jumanne usiku, bunge la Israeli-Knesset, lilivunjwa moja kwa moja kulingana na sheria baada ya makataa ya mwisho kupita ya kuidhinishwa kwa bajeti ya mwaka 2020.

Jaribio la saa 11 la kuepuka kuvunjwa kwa bunge lilishindwa baada ya muswada wa kurugusu kuongezwa kwa muda wa majadiliano zaidi kupingwa kwa kura, kinyume na ilivyo tarajiwa.

Saa kadhaa kabla ya muda wa mwisho kumalizika, Netanyahu, ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la mrengo wa kulia la chama cha Likud , na mpinzani wake wa kisiasa Benny Gantz kutoka vuguvugu la mrengo wa kati la Blu na nyeupe , walilaumiana kila upande ukiutuhumu mwingine kusababisha mzozo huo.

“Sikutaka huu uamuzi ,” Netanyahu aliwaambia waandishi wa habari. “Likud haikutaka huu uchaguzi . Tumechagua tena na tena dhidi ya uchaguzi. Bahati mbaya , Benny Gantz alivunja makubaliano yake na sisi .”

Alisema Likud kitapata “ushindi mkubwa” katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Machi.

Gantz alisema kuwa kauli za waziri mkuu Netanyahu ni za “uongo zaidi kuliko maneno “. Alisema kuwa Netanyahu alitaka kusababisha uchaguzi kwa lengo la kuepuka kesi yake ya ufisadi.

Wawili hao waligawana madaraka tangu mwezi Aprili katika muungano ambao haukua rahisi , wakikubaliana kupokezana madaraka na waziri mkuu, ambapo Netanyahu angechukua mamlaka kabla ya kipindi cha kukabidhi madaraka kwa Gantz mwezi wa Novemba 2021.

Wachambuzi wanasema mgawanyiko ulikuwa njia ya Netanyahuya kumaliza muungano kutokana na pengo katika mkataba ambao kwa mujibu wake uwaziri mkuu utakabidhiwa kwa kiongozi mwingine kwa kipindi cha miezi mitatu kama chochote kingesababisha uchaguzi, kando na tukio la kushindwa kupitishwa kwa bajeti.

Kura za maoni za hivi karibuni zinaonesha kuwa chama cha Blu na Nyeupe- Blu and White kimesambaratika , na huku uungaji mkono wa Likud ukipungua kitarejea kama chama kikubwa zaidi.

Hatahivyo Netanyahu anakabiliwa na shinikizo kubwa, huku maandamano ya mitaani dhidi ya utawala wake, kesi ya ufisadi ikitarajiwa kufufuliwa tena mwezi Januari, na mapambano yanayoendelea dhidi ya maambukizi ya corona kote nchini.

Baadhi ya wachambuzi wanasema alitaka uchaguzi kabla ya kukabidhi madaraka kwa Gantz, lakini angependelea hilo lifanyike baada ya mwezi Machi. Hilo lingetoa muda zaidi kwa ajili ya kampeni ya utoaji wa chanjo ya corona na wakati ambapo uchumi utakuwa umeanza kufufuka.

Netanyahu pia anakabiliwa na changamoto mpya kutoka chama cha mbunge wa zamani wa Likud , Gideon Saar, ambaye ameunda chama cha mrengo wa kulia ambacho kimeazimia kukipunguzia kura ngome ya kisiasa ya Netanyahu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here