Iran: Mwandishi wa habari mkosoaji anyongwa

0

TEHRAN, Iran

IRAN jana Jumamosi imemnyonga mwandishi wa blogu na mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Tehran, Ruhollah Zam licha ya mara kadhaa kuomba kupewa msamaha.

Taarifa za kunyongwa kwa Zam zimetolewa na Shirika la Habari la IRNA na kuthibitishwa na wizara ya sheria ya nchi hiyo.

Zam alihukumiwa kifo na mahakama moja mjini Tehran mnamo mwezi Juni kwa makosa ya kuendesha propaganda dhidi ya utawala wa Iran pamoja na kuchochea maandamano ya umma kupitia tovuti yake ya Amad News.

Mwanablogu huyo kwa sehemu kubwa alikosoa kile alichokitaja kuwa udanganyifu katika Uchaguzi wa Rais wa mwaka 2009 uliowezesha Rais wa Zamani wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad kuchaguliwa tena.

Ufaransa na Ujerumani zimeelezea kufadhaishwa na taarifa za kunyongwa kwa Zam na kuitaja hukumu hiyo kuwa ya kikatili na inayotishia uhuru wa habari kwenye Jamhuri hiyo ya Kiislamu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here