INFINIX WANAKULETEA SIMU MPYA MJINI ‘HOT 10 PLAY’ YENYE GUMZO YA KIPEKEE

0

Tumezoea kuona kampuni ya simu ya Infinix kuja na vitu vipya kila mwanzoni mwa mwaka na sasa tunaelekea kuumaliza mwezi huu wa kwanza pasipo kuona pirikapirika ya aina yoyote yenye kuashiria ujio wa simu mpya nchini Tanzania huku nchi kama Nigeria tayari wameshazindua simu mpya Infinix
HOT 10 play. Uchelewaji wa Simu hiyo mpya unazua maswali mengi mitandaoni moja wapo ikiwa nini sababu ya simu
hiyo kuchelewa nchini kwetu, lakini kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari kama vile mitandao ya kijamii inavyodai kwamba Infinix HOT 10play iliyozinduliwa Nigeria ama nchi nyengine za jirani ni tofauti itayotufikia watanzania.

HOT 10play zipo za aina tofauti zenye kutofautiana ukubwa upande wa memory (128 + 4, 64 + 4 na 32 +2) na hili ndio huenda inapelekea Infinix HOT 10play simu yenye kusemekana kuwa na battery yenye
mAh 6000 kuchelewa sokoni.

Vile vile kuna wadau wa Infinix wenye kufuatilia kiundani bidhaa zao wanadai Infinix haijawai kuwaangusha na wanachofahamu wao mara nyingi Series pendwa ya Infinix HOT 10 utambulisho/ujio
wake huambatana na campaign za sikukuu ya wapendanao ili kuashiria upendo kwa wateja wao hivyo basi tutegeemeni Infinix HOT 10play wakati wowote kuanzia sasa.
Tembelea https://www.infinixmobility.com/tz/ kufahamu mengi zaidi kuhusiana na bidhaa zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here