India yapeleka neema Nepal

0
Balozi wa India nchini Nepal, Vinay Mohan akiwa na Waziri wa Fedha wa Nepal, Bishnu Prasad-Paudel

NEW DELHI, India

INDIA imezidi kung’ara kwenye siasa za kimataifa na kukuza diplomasia yake ya uchumi, baada ya serikali ya Waziri Mkuu, Narendra Modi kuhakikisha inatoa misaada mbalimbali kwenye nchi Duniani.

Kitendo cha serikali hiyo, kutoa msaada nchini Nepal wa ujenzi wa makazi bora kupitia kwa  Balozi wake, Vinay Mohan Kwatra kumetajwa ni moja ya mipango madhubuti ya ujenzi wa diplomasia kwa nchi hiyo.

Balozi huyo, alikabidhi hundi ya NPR bilioni 1 kwa serikali ya Nepal kama malipo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba wa Nepal.

Balozi wa India Kwatra alikutana na Waziri wa Fedha Bishnu Prasad Paudel na kumkabidhi hundi hiyo.

“Kulikuwa na mazungumzo mazuri ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa nchi mbili wa uchumi na maendeleo kati ya nchi hizi mbili kwa ustawi na maendeleo na siasa za Nepal na India,” anasema Balozi Kwatra.

Anaongeza “Nilitumia fursa hii pia kutoa hundi ya NPR bilioni 1 kama sehemu inayofuata chini ya miradi ya ujenzi wa nyumba iliyofadhiliwa na India huko Gorkha na Nuwakot,”

India ilikuwa imetangaza mpango wa ujenzi huko Nuwakot na Wilaya ya Gorkha ya Taifa la Himalaya baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi la 2015. India imeahidi kujenga jumla ya nyumba 50,000 katika wilaya mbili ambapo UNDP na UNOPS wanapeana msaada wa kiufundi na mashauriano mengine.

Serikali ya India ambayo imekuwa ikitoa mkono wake katika ujenzi wa nyumba huko Nepal imeshirikiana na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Huduma za Miradi (UNOPS) kwa kutoa Uwezeshaji wa Kijamaa na Ufundi kwa wamiliki wa nyumba kwa kuhakikisha kuwa wanajenga tena nyumba zao kulingana na serikali ya kanuni za kukabiliana na tetemeko la ardhi la Nepal. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here