Ifahamu historia ya mwanamuziki wa reggae Peter Tosh

0

NA MWANDISHI WETU

OKTOBA 19, 1944 alizaliwa msanii wa muziki wa reggae raia wa Jamaica Peter Tosh. Jina lake halisi lilikuwa ni Winston Hubert Mclntosh.

Peter Tosh alikuwa ni mwanamuziki Mjamaika wa mtindo wa rege, alikuwa na kipaji mahiri cha kutunga mashairi ya muziki, pia alikuwa ni mpigaji mahiri wa gitaa.

Peter Tosh alikuwa mtoto pekee wa mama Alvera Coke, baba yake aliitwa James Mclntosh ambaye alikuwa ni mhubiri wa kanisa la Savanna-la-mar.

Katika maisha yake hakubahatika kulelewa na baba na mama yake, alilelewa na shangazi yake sababu wazazi wake hawakuwa na muda wa kumlea.

Alijitunza mwenyewe kwa baadhi ya mambo bila kupata matunzo kutoka kwa baba yake ambaye alikuwa ni baba wa watoto wengi.

Peter Tosh alianza kupiga ala za muziki akiwa kijana wa umri mdogo, alijifunza kupiga kinanda kwa miezi sita pia alijifunza kupiga gitaa, ala hiyo ndiyo iliyo kuja kumpa umaarufu, mwaka 1956 baada ya kuondoka Savanna-la-mar Peter na shangazi yake walikwenda mji wa Denham katika jiji la Kingston.

Peter Tosh alipofikia umri wa miaka 15 shangazi yake alifariki, hivyo alikwenda kwa mjomba wake West Road huko Trench Town. Peter alikutana na Robert Nesta Marley (Bob Marley) na Neville O’Reilly Livingston (Bunny Wailer) na wakauunda utatu wa kwanza wa Wailer halisi na wakajiita Wailin’Wailers, na walianza kuimba pamoja mwaka 1962 na alikuwa ni yeye tu kati yao aliyeweza kupiga ala, hivyo alifanya bidii ya kuwafundisha wenzake na alikuwa ni mmojawapo aliyemfundisha Bob kupiga gitaa.

Bob Marley

Wakiwa ndani ya kundi hilo Peter alimaliza kazi ya kumfundisha Bob kupiga gitaa mwaka 1962.

Ukiwaondoa watatu hao pia kundi hilo lilikuwa na waimbaji wengine wa nyuma kama Junior Braithwaite, Beverley Kelso na Cherry Smith.

Wimbo wa kwanza wa The Wailers ulijulikana kama “Simmer Down” wimbo huop uliwapatia mafanikio ambapo mwaka 1965 waliondokewa na wanamuziki wao akina Braithwaite, Kelso na Smith.

Mwaka 1966 Marley na mama yake walihamia Marekani na kukaa miaka miwili na kurejea Jamaica mwaka 1967 ambapo akina Tosh walikuwa wakiendelea kuwakilisha kundi hilo.

Peter Tosh alijitoa Wailers mwaka 1974 hii ni baada ya Chris Blackwell kukataa kutoa albamu yake ya kwanza yeye akiongoza safu ya uimbaji.

Peter Tosh aliuawa nyumbani kwake mwaka 1987.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here