Idriss Sultan afanikisha kurudisha Dola 300, 000 alizozipoteza

0

NA MWANDISHI WETU

MCHEKESHAJI Idris Sultan ambaye pia ni mfanyabiashara amedai kuwa amefanikiwa kuzirejesha Dola Laki 3 (zaidi ya Milioni 500) alizoshinda Big Brother Africa mwaka 2014 nchini Afrika Kusini.

Inaelezwa fedha hizo zilipotea baada ya kuwekeza kwenye miradi ambayo haikuweza kuzaa matunda kutokana na kukosa uangalizi mzuri, huku mwenyewe akidai watu wake wa karibu ndio waliomwangusha.

Akizungumza katika kipindi cha Empire cha E FM Redio, Sultan amesema fedha hizo alifanikiwa kuzirejesha rasmi mwaka 2018 baada ya kufanya kazi kwa bidii na kuanzisha miradi mbalimbali.

“Ile dola laki tatu, nimekuja kuipata tena 2018, hiyo ni miaka minne baadaye, siku hiyo naenda Benki wananiambia umetimiza dola laki tatu yako, wakaanza kunipigia makofi, ndio maisha,” amesema Sultan.

Ameongeza kuwa alipoenda Big Brother hakuwa na mpango kupata fedha, bali kupata ‘platform’ halafu aitumie kufanya vitu vyake vikubwa sana na ndio kitu anafanya hadi sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here