Hawa hapa wachezaji 10 bora wa EPL

0

LONDON, UINGEREZA 

BILA shaka umekuwa msimu wa kusisimua kwa Southampton na Danny Ings.

Timu hiyo imeingia kwenye timu nne bora za Ligi ya Premier kwa usaidizi wa mabao 5 kutoka kwa mshambuliaji Ings, ambaye amechaguliwa kuwa bora na mashabiki wa BBC Spoti .

Wastani wa magoli kutoka kwa mashabiki wa BBC Spoti, wachezaji wanne wa Ralph Hasenhuttl wameingia kwenye timu ya wachezaji 10 bora huku wachezaji wa Southampton wakichaguliwa katika kila kitengo.

Wachezaji walihitajika kuwa wamecheza angalau mechi nne msimu huu kwa wao kujumuishwa.

Wachezaji 10 bora

Ings ndiyo anayeongoza na huenda angejumuishwa kwenye kikosi cha England katika michuano ijayo ya kimataifa ikiwa hangepata jeraha la goti.

Beki wa Leicester Christian Fuchs pengine huenda ndio jina linaloshangaza wengi katika orodha hiyo ya wachezaji 10 bora.

Mchezaji huyo 34 alitaka kuondoka Foxes mkataba wake ulipokamilika mwezi uliopita lakini kuendeleza mkataba wake kwa mwaka mmoja inaonekana kuwa hatua ya kutia moyo kwa kocha Brendan Rodgers.

Walinda lango 10 bora

Mchezaji mpya wa Chelsea Edouard Mendy ndiyo mlinda lango wa Ligi ya Premier ambaye amefurahisha wachezaji wengi msimu huu.

Mlinda lango wa Leeds Illan Meslier na wa Newcastle Karl Darlow pia nao wamekuwa na mchezo mzuri wa kuwawezesha kuingia ndani ya kundi la 10 bora.

Mabeki 10 bora

Fuchs amekuwa na mwanzo mzuri na haishangazi kuona mwenzake wa Leicester Timothy Castagne yule aliyechukua nafasi yake Ben Chilwell wa Chelsea pia nao wameingia kwenye kundi hilo.

Licha ya Brighton kuwa katika nafasi ya 16, Tariq Lamptey amekuwa nyota katika timu ya Seagulls.

Washambuliaji 10 wa kati

Jannick Vestergaard na Jan Bednarek wa Southampton wote wameingia kwenye timu 10 bora baada ya kuanza vyema.

Tyrone Mings na Ezri Konsa wa Aston Villa ni wachezaji wengine matata sana kama ilivyo kwa Thiago Silva wa Brazil, waliotia saini makubaliano ya bila malipo na Chelsea.

Viungo wa kati 10 bora

Wachezaji viungo wa kati wa Southampton wanachukua nafasi tatu za juu pamoja na bingwa wa free-kick James Ward-Prowse wakiwa ndio wanaosemekana kuchukua nafasi za juu wakifuatiwa na mchezaji wa kimataifa wa Scotland Stuart Armstrong na Mhispania Oriol Romeu.

Pia umekuwa mwanzo mzuri kwa nahodha mshindi wa tuzo Jordan Henderson ambapo mchezo wake kwa Liverpool hadi kufikia sasa umemuwezesha kuchukua nafasi ya 9.

Winga 10 bora

Akiwa amefunga mabao 10 na kusaidia mara tano hadi kufikia sasa, Jack Grealish wa Villa anaongoza kwenye orodha hiyo huku mchezaji wa Everton raia wa Colombia James Rodriguez pia naye akionesha mchezo mzuri.

Washambuliaji 10 bora

Sadio Mane, Patrick Bamford na Calvert-Lewin wameingia kwenye kundi la 10 bora.

Lakini pia Rodrigo aliyesajiliwa na Leeds naye ameshika nafasi ya 9 licha ya kufunga goli moja tu hadi kufikia sasa msimu huu.

Mshambuliaji wa Villa Ollie Watkins ameorodheshwa juu zaidi ya mwingine yoyote akiwa na wastani wa alama 9.3 kwa mbwembwe zake walipoiadhibu mabingwa Liverpool 7-2.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here