Harusi iliyohudhuriwa na watu 10,000 waliokaa ndani ya magari

0

NA MWANDISHI WETU

Janga la virusi vya corona limewaathiri kwa kiasi kikubwa wapendanao ‘ambao wamekuwa na ndoto ya kufanya harusi kubwa.

Lakini wapenzi wa Malaysian wameweza kuepuka masharti ambayo yangewaruhusu kuwaalika wageni 20 tu kwenye harusi yao na badala yake wamefanikiwa kuwakaribisha watu 10,000 harusi yao, na kwa kuzingatia masharti ya Covid-19

Si jambo la kawaidi, unaweza kusema. Lakini linawezekana, kama utaweza kuifanya harusi yako liwe tukio la kupitiwa na watu.

Jumapili asubuhi , maharusi walikuwa meketi nje ya jengo kubwa la serikali katika mji wa Putrajaya, kusini mwa mji mkuu wa Malasyia Kuala Lumpur, huku wageni wakipita taratiibu ndani ya magari yao.

Madirisha ya magari yalifungwa na wageni hawakusogelea kabisa maharusi kwahiyo walichofanya ni kuwapungia mikono na kuwaonesha japo tabasamu katika siku hiyo ya harusi yao.

Huenda ikawa sio sawa na harusi za kawaida ulizozizowea, lakini Bwana harusi Tengku Muhammed Hafiz na Bi harusi Oceane Alagia sio maharusi sawa na wale unaowaona kila mara.

Bwana harusi ni mtoto wa mwanasiasa mwenye ushawishi na waziri wa zamani Tengku Adnan – ambaye pia salikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa katika siku hiyo ya Jumapili.

“Nimefahamishwa kuwa kulikuwa na magari zaidi ya 10,000 hapa tangu asubuhi, aliandika baba yake bwanaharusi ambaye alishirikisha umma picha za harusi kwenye ukurasa wake wa Facebook:

“Mimi na familia yangu tumeheshimiwa sana. Asanteni sana nyote kwa kuelewa na kuheshimu taratibu zote zilizotimizwa na wageni wapita njia waliohudhuria harusi bila kutoka nje ya magari .”

Ilichukua muda wa saa tatu hadi kwa wageni wote washiriki wa harusi hiyo kuwa wamekamisha shughuli ya kupita ndani ya magari yao kando na eneo walipokuwa wameketi maharusi.

Hatahivyo, walipata zaidi ya mkono wa heri, waliweza pia kusikia neno -asante kutoka kwa maharusi waliowashukuru walau kwa kupitia kwenye harusi yao.

Kwa kuzingatia maagizo ya kutokaribiana, wageni walipata chakula cha jioni-ingawa walilazimika kuchukua chakula ambacho waliandaliwa mapema na wakagawiwa kupitia kwenye madirisha yao ya magari , huku magari yakiendeshwa taratiibu , kulingana na vyombo vya habari vya Malaysia.

Harusi ya Roma Popat na Vinal Patel (pichani) pia ilihudhuriwa na wageni waliokaa ndani ya magari yao nchini Uingereza

Sherehe hizo zilifanyika siku moja kabla ya baba yake na bwanaharusi ambaye ni mwanasiasa kupatikana na kesi ya rushwa ya dola 500,000 (£370,000) na kuhukumiwa kifungo cha miezi 12 jela na kulipa faini.

Malaysia kwa sasa inapambana na wimbi jipya la maambukizi ya Covid-19. Kwa ujumla nchi hiyo ilikuwa imetangaza jumla ya visa 92,000 cna zaidi ya vifo 430 vilivyosababishwa na janga hilo.

CHANZO: BBC

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here