Haruna Moshi ‘Boban’ apongezwa kujiunga na ukocha

0

NA SHEHE SEMTAWA

BAADA mchezaji wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara Haruna Moshi ‘Boban’ kuwaamua kuwa kocha, baadhi ya wachezaji wa zamani wamemtabiria makubwa katika jukumu lake hilo jipya.

Ikumbukwe Boban aliwahi kuzichezea Simba na Yanga kwa mafanikio makubwa hivi sasa anaifundisha…

Akimzungumzia mchezaji huyo, Kiungo aliyewahi kuzichezea Simba na Yanga, Athuma Iddi ‘Chuji’ alisema Boban anafaida kubwa kwa sababu alipitia changamoto nyingi katika kipindi chake cha uchezaji.

“Kwa mtazamo wangu mimi aliyecheza anatakiwa kupewa uongozi sasa kwa Haruna kwa kitu kama hicho naamini atasaidia wengi sana na atafanya vizuri.

“Huo ni mwanzo tu yani kwa sababu kapitia mengi na anajua mpira wetu jinsi ulivyo kiasi kwamba atawasaidia vijana wetu wanaokuja hivi sasa,”alisema Chuji.

Nizar Khalfan aliyewahi kucheza naye pamoja, alisema kuwa alifurahishwa na ujio wa Harouna katika kazi ya ukocha wa mpira wa miguu ambapo Nizar kwa sasa ni Mwalimu wa Timu ya African Lyon.

“Hicho kitu kizuri kwa sababu, ukiangalia wengi wetu tumecheza mpira kwa hiyo uamuzi wake uko sahihi.

“Unajua ni vizuri ukitoka kucheza mpira ili uweze kuwaelekeza vijana kwa sababu vijana wengi wanakosa watu sahihi wa kuwaelekeza mpira kwa hiyo nadhani ukiingia moja kwamoja kufundisha inakuwa kitu kizuri zaidi.

“Kwa sababu wakati mwingine inategemea kwa mtu mwingine alicheza mpira lakini ana uwelewa mpira, mtu aliyecheza mpira anakuwa na vitu vingi vya kusaidia mchezaji kwa sababu amepitia mambo mengi kwa sababu amecheza na vitu vingi ameviona.

“Kwa hiyo uzoefu wake aliopata inakuwa ni vizuri kuwaelekeza wachezaji wake aliokuwa nao, inasaidia sana Harouna alikuwa mchezaji mzuri kila mtu anajua hilo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here