Harmonize atangaza bifu na Kondeboy wa Simba

0

NA MWANDISHI WETU

MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo fleva na Mtendaji Mkuu (CEO), wa Lebo ya Konde Gang, Rajab Kahali ‘Harmonize’ wikiendi alijikuta katika hali ya tafrani baada ya kukataza watu kutumia jina la Kondeboy kwa mchezaji wa Simba akidai linatumika kimakosa kwani ni jina lake na angeombwa kulitumia.

Baada ya Ujumbe aliopost mchambuzi wa soka Tanzania Shaffih Dauda ya kuwaomba mashabiki wa soko kutoa maoni yao kuhusu kiwango cha mchezaji wa Simba, Luis Miquissone katika mchezo dhidi ya FC Plateau ya Nigeria na mashabiki kuanza kutoa maoni yao ndipo Harmonize alipokuja ‘ku-comment’ akizungumzia jina hilo.

“Baba hilo jina is a brand (ni chapa)usiligawe bila makubaliano, ana mtoto anaitwa Zurekha umeongea naye mmekubaliana kuuza jina la baba yake ? alihoji Harmonize.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here