HAJI MANARA AWAPIGA ‘STOP’ MASHABIKI WA YANGA MECHI YA SIMBA VS PLATEU

0

Klabu ya Soka ya Simba imesema haitaruhusu Shabiki wa Klabu ya Yanga kuingia katika mchezo wao wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United mchezo utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo, Haji Manara amesema watazuia kuingia shabiki wa timu hiyo kutokana na mechi hiyo ni ya kwao.


“Mechi hii ni ya kwetu sio ya hisani, kama unataka kuzomea tulia nyumbani au ishia pale Mianzini au Keko”, amesema Manara.

Manara amesema endapo mashabiki hao wataingia katika uwanja huo, amewaasa mashabiki wa Simba SC wasiwafanyie vurugu na kuwapiga, amewaomba Mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuishangalia timu hiyo.

“Plateau United sio timu ya kubeza, tunataka tucheze Soka tuwaburudisha Wana Simba na kuwafunga katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, tutumie vizuri nafasi ya CAF kuruhusu Mashabiki Elfu 30 kuingia Uwanjani”, ameeleza Manara.

Simba SC itarudiana na Plateau United Desemba 5, 2020 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa mjini Jos nchini Nigeria kuondoka na ushindi wa bao 1-0.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here