Gondwe aagiza mameneja kuwekwa rumande

0

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe ameamuru kukamatwa na kuwekwa rumande kwa wasimamizi na mameneja wa ghala la kuhifadhia kemikali lililopo Mbande Kisewe Dar es salaam, baada ya kugundulika kuwa ghala hilo halikusajiliwa.

DC Gondwe ametoa maagizo hayo katika operesheni ya ukaguzi wa maghala ya kuhifadhi kemikali inayoendelea Wilaya ya Temeke, akiwa na maofisa kutoka  Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Licha ya ghala hilo kutosajiliwa, DC Gongwe amebaini kuwa kulikuwa na shehena za kemikali mbalimbali zilizoisha muda wa matumizi na kuwekwa upya katika mifuko kisha kuingizwa sokoni kinyume na sheria.

DC Gondwe ametaka  ghala hilo kuwa chini ya usimamizi kwa ajili ya hatua nyingine zikiwemo kuharibu kemikali hizo chini ya uangalizi wa serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here