Fahamu vyakula vinavyoweza kuimarisha tendo la ndoa

0

Na Mwandishi Wetu

KAMA kungekuwa na ushahidi kwamba chakula cha aina moja kinaweza kuimarisha tendo la ndoa na kukuzidishia hamu, huenda kungekuwa na uhaba wa chakula hicho.

Lishe bora, kufanya mazoezi na afya nzuri ya akili yote yanaweza kuimarisha tendo la
ndoa. Lakini kuna vyakula vyovyote maalum vinavyoweza kukuongezea hamu ya tendo
la ndoa? Viungo vinavyoweza kuchochea hisia ya furaha- kutokana na homoni ya endorphins, vina virutubisho vinavyohusishwa na kuimarika kwa tendo la ndoa, au kwa jumla vinahusishwa na utajiri na ufanisi na mara nyingi hutajwa kuwa vichochezi vya
kuimarisha tendo hilo la ndoa.

Manufaa ya kula chaza au kombe?

Casanova, mpenzi maarufu katika historia inaarifiwa alikuwa chaza 50 wakati wa
kiamsha kinywa.

Hata hivyo hakuna uthibitisho baina ya kula chaza na kuongezeka kwa tendo la ndoa,
basi uvumi ulitoka wapi?

Simulizi au ngano za kale zinaeleza kwamba wakati Aphrodite – Mungu wa tendo la
mapenzi – alipozaliwa kutoka povu jeupe na kufufuka kutoka baharini ndipo chakula cha
baharini kilipoonekana kuwa ni kichochezi cha kuimarisha tendo la ndoa.

Lakini kuna habari nzuri kwa wanaopenda kula chaza, wana madini ya zinc kirutubisho
muhimu kinachotumika kuunda homoni ya testosterone.

Utafiti umebaini kwamba zinc inaweza kusaidia kutibu matatizo ya wanaume kuweza kuzalisha na huenda zinaweza kuongeza ubora wa manii.

Vyanzo vingine vizuri vya zinc hupatikana katika nyama nyekundu, mbegu kama za tango na sim simu, korosho na lozi lakini pia maziwa na hata jibini.

Chokoleti inaweza kukufanya mpenzi mzuri?
Kula chokoleti nyeusi kunaweza kukupa hisia ya awali unapompenda mtu, kwa mujibu
wa utafiti, kwasbaabu ina ina 'kemikali ya mapenzi' phenylethylamine (PEA).

PEA – ambayo huwepo katika miezi ya kwanza ya mahusiano – huchangia kuwepo kwa
homoni inayomfanya mtu kujihisi vizuri na kuchochea raha katikati mwa ubongo.

Ni kiwango kidogo tu cha PEA kipo katika chokoleti na kuna shaka iwapo kiwango hicho
kinaendelea kuwepo wakati kinaliwa.

Cocoa pia ina amino acid tryptophan, na husemekana kuongeza msukumo wa damu na
viwango vya serotonin (homoni nyingine ya furaha).

Basi uhusiano baina chokoleti na tendo la ndoa ulianza vipi? Huenda ni katika karne ya
16.

Hernán Cortés alikuwa mtawala wa Kihspania katika karne hiyo aliyeithibiti
inayojulikana hii leo kama Mexico chini ya ufalme wa Castile.

Inadhaniwa ndio raia wa kwanza Ulaya kugundua chokoleti. Alimuandikia barua mfalme
akimueleza kwamba amegundua kinyaji cha cocoa kinasaidia "kuimarisha kinga na
kukabiliana na uchofu".

Lakini raia wa zamani wa Castile huenda walihusisha nguvu hizo na chokoletina hakuna
uhakikisho kuunga mkono ushahidi wa kuimarisha tendo la ndoa.
Pilipili kuchangamsha tendo la ndoa?

Pilipili zina kinachojulikana kama capsaicin, ambayo utafati umeaini inaweza kuchochea
homoni ya endorphins (ya kujihisi furaha).

Husaidia pia kuharakisha ufanyaji kazi mfumo wa kusaga chakula tumboni na huongeza
ujoto mwilini na kasi ya moyo unavyopiga, mambo ambayo huwa tunayahisi wakati wa
tendo la ndoa.

Lakini hakikisha kwamba unakumbuka kuosha mkono unapotayarisha pilipili!

Pombe husaidia au hutatiza?

Pombe inaweza kuongeza hamu kwa kuondosha kujizuia, lakini kama anavyoeleza
Macbeth wakati akiwa amelewa, “huchochea hamu, lakini huondosha uwezo”.

Hisia hupungua kwa wanaume na wanawake kwa kunywa pombe nyingi, na katika
kipindi cha muda mrefu inaweza kupunguza uwezo wako wa kushiriki tendo la ndoa na
hata mara nyingine katika hali mbaya zaidi kuchangia matatizo ya kushindwa kabisa
kushiriki tendo hilo.

Zaidi ya hapo harufu ya pombe haivutii!

Vichochezi vya kuongeza hamu

Vichochezi vinaweza kugawanywa katika makundi matatu.

Vinavyoshughulikia hamu, uwezo wa kushiriki tendo na raha inayotokana na tendo
lenyewe.

Hakuna vilivyothibitishwa kisayansi kuwana uwezo wa kufanya kazi kwa binaadamu ,
kutokana na ugumu wa kupima ufanisi

Ni harufu ya kuiva na kuoza kwa tunda pekee ndiyo iliyoweza kuthibitishwa, na hufanya
kazi kwa wadudu wa matunda wanaoruka.

Dk. Krychman, mtaalamu wa afya ya ngono anasema anadhani watu hula vichochezi
hivyo kwasababu ya imani kwamba vitafanya kazi, na anauliza iwapo jambo
linakusaidia, je unajali kwanini inafanya kazi?

Vichochezi vingi huwa ni vinywaji, lakini imeshauriwa kuepuka dawa zinazotokana na
mimea iwapo hazina taarifa ya usalama au yoyote inayotajwa kuwa ya miujiza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here