Fahamu umuhimu wa kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja

0

NA MWANDISHI WETU

Mara nyingi uhusiano huchukuliwa kuwa kati ya watu wawili tu. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba utamaduni huu sasa unaanza kutiliwa mashaka na kuchunguzwa kwa undani huku watu wakitafuta mbinu zao za kujifafanulia mapenzi ni nini.

Mshiriki mmoja wa kipindi cha kwenye televisheni Uingereza Amy Hart, anasema anajua kuwa mume wake ana mahusiano ya mapenzi ya siri ya nje ya ndoa yao.

Bi. Hart anasema kwake yeye aliamini kuwa mapenzi ni ya watu wawili lakini mume wake alivunja utamaduni huo.

Ni baadhi tu ya mfano inayopelekea watu kuamini kuwa ukiwa katika ndoa huru huenda kukafanya washirika kuwa na uhuru wa kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa.

Katika mahusiano yaliyo huru, wanandoa hujadiliana na kukubaliano mipaka yao.

Hata hivyo, ndoa zinazochukuliwa kuwa za mpenzi mmoja, mambo kama hayo hayawezi kujadiliwa.

Hata hivyo, licha ya kwamba mara nyingi watu huchukulia wapo katika makubaliano ya ndoa ya mke mmoja, utaona wahusika hupendelea kuwa na uhusiano wa mapenzi na watu wa nje badala ya wawili waliofunga pingu za maisha.

Ndoa ya mke uji uleta majuto kwa wengi

“Ukiangazia aina mbalimbali za uhusiano uliopo, asilimia 5 inaweza kubainishwa kama wa zaidi ya mpenzi mmoja,” amesema Amy Muise, profesa msaidizi wa masuala ya saikolojia katika chuo kikuu cha York Toronto, Canada.

“Katika maisha ya mwanadamu, asilimia 21 ya watu wamewahi kujihusisha na mapenzi nje ya ndoa.”

Hata hivyo, katika kipindi hiki cha virusi vya corona, watu wamekuwa na mazingira magumu ya kukutana na wapenzi wa kando nje ya majumba yao kwasababu ya hatua zilizochukuliwa na nchi mbalimbali kudhibiti virusi vya corona kama kutokaribiana.

Hatua hii huenda ikalazimisha walio na mahusiano ya mapenzi nje ya ndoa zao kusalia na wenza wao majumbani kwa kipindi kirefu.

Na pia saikolojia ya kijamii inaonesha kuwa kuna sababu zinazofanya watu kuamini uhusiano wa nje ya ndoa una faida.

Wataalamu wa masuala ya ndoa wanasema idadi ya ndoa zilizovunjika ni kubwa kuliko takwimu zilizopo.

Zamani za kale inaaminika kwamba watu waliishi katika makundi madogo ya kifamilia kwa pamoja.

Wakati huo ambapo wanaume wengi waliaminika kuwa wawindaji, walikuwa waaminifu kwa mke lakini akipata mtoto anatafuta mpenzi mwingine.

Mtindo huo huenda unaelezea kwanini wanaume siku hizi wanapendelea sana uhusiano unaowaacha kuwa huru.

Kulingana na utafiti uliofanywa na mwanasaikolojia Justin Lehmiller juu ya mahusiano ya watu, wanaume wengi wanapendelea sana kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja ikiwa ni asilimia 26 ikilinganishwa na asilimia 8 ya wanawake.

Sasa hivi ndoa nyingi zinajiweka katika ile hali ya kutokuwa na mapenzi ya nje ya ndoa ingawa hali halisi ni tofauti hata ukirejelea agano la kale kuna mifano mingi ya walioa wake zaidi ya mmoja.

Lakini je kwanini sasa hivi wanaume wengi wanaonekana kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa?

Ni vigumu kusema bila kusingizia sanaa, utamaduni na kadhalika.

“Mara nyingi, wakati tunakua wazazi wetu walikuwa wameoa na kuwaona wapo katika ndoa ya mke mmoja.”

“Tangu watu walipoanza kujichukulia vipande vya ardhi na kudai kuwa ndio wamiliki, ndoa zilikuwa moja ya njia ya kudhibiti mali na kuimilikisha familia na kuanzia wakati huo, ndoa imeanza kuonekana kuwa jambo la msingi.”

Utafiti unaonesha kuwa wanandoa wenye maslahi tofauti ya mapenzi wako vizuri zaidi wakiwa na wapenzi zaidi ya mmoja.

“Katika uhusiano mara nyingi huwa kuna utofauti wa maslahi kati ya watu wawili,” anasema Muise mtaalamu wa masuala ya mahusiano. “Hatahivyo, watu wenye mpenzi zaidi ya mmoja huenda wakawa ni wenye kutimiza haja zao zaidi.”

Aidha, inasemekana katika utafiti mmoja, kwa watu waliotaka kuwa na uhusiano huru na kufanikiwa, walihisi kufanikiwa kutimiza mahitaji yao.

”Maisha mazuri ya uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wa nje yanamfanya mwanaume kuhisi anatosheka na mpenzi wake halali kwasababu ghafla ile shinikizo ya kuwa mtu mmoja atimize kila kitu kumfurahisha mwenza wake inaondoka”, amesema Joel.

Ulaya

“Kunapokuwa na furaha katika uhusiano wa kimapenzi, wanandoa wanaweza kuwasiliana kwa ubora zaidi,” Joel anasema.

“Lakini pia ni vigumu kutimiza uhusiano huru ikiwa huwezi kutimiza masharti muliokubaliana.

Aidha, kuridhika kihisia – kujihisi salama, na kuwa na ukaribu – kunaonekana kuendelea kuongezeka kadiri muda unavyoendelea. Wakati huohuo kuwa huru, kujihisi kuwa na furaha nako kunapungua ikiwa ni ndoa ya mke mmoja.

“Mwanzoni maisha huwa ni matamu na mapenzi tele lakini inafika wakati munaanza kutabirika,” anasema Rhonda Balzarini, mwanasaikolojia wa chuo kikuu cha York.

Balzarini anatoa mfano wa mke halali aliyeolewa anakuwa na majukumu mengi yake binafsi, kuangalia nyumba na watoto ilihali mke wa nje mara nyingi hana majukumu hayo na hivyo basi atakuwa na muda mwingi wa kuendeleza mahusiano ya mapenzi. (Chanzo: BBC)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here