ETHIOPIA KUWAREJESHA WAKIMBIZI WA TIGRAY

0

Maelfu ya wakimbizi waliokimbia kwenye kambi zao katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, baada ya kambi zao kushambuliwa kwenye mapigano baina ya majeshi ya Serikali na waasi wa kundi la TPLF, wameanza kurejeshwa, kwa mujibu wa serikali ya Ethiopia.

Taarifa iliyotolewa leo inasema kuwa operesheni yake dhidi ya kundi la TPLF haikuwa kitisho cha moja kwa moja dhidi ya wakimbizi hao, ambao wamehifadhiwa kwenye jimbo la Tigray.

Wakimbizi 96,000, wengi wao wakiwa raia wa nchi jirani ya Eritrea walitajwa kwenye ripoti ya Umoja wa Mataifa siku chache zilizopita kwamba wako hatarini.

Umoja huo ulionya kwamba endapo taarifa za kushambuliwa kwa wakimbizi zitathibitishwa, basi utakuwa uvunjwaji mkubwa wa taratibu za kimataifa.

Hayo yanakuja wakati mashirika ya kimataifa yanayotowa misaada ya kibinaadamu yakisema kwamba wafanyakazi wake wanne wameuawa kwenye vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe vya Tigray.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here