Esma:Sijatoa mimba,nilipungukiwa damu

0

NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM

ESMA Khan almaarufu kama Esma Platnumz, ni dada wa supastaa wa Bongo Fleva, Afro-Pop na Afro-Beat, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Esma amejizolea ustaa kupitia mgongo wa Diamond kutokana na tabia yake ya kuingilia uhusiano wa kimapenzi wa kaka yake huyo.Kutokana na ishu hiyo, Esma ambaye ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti), amepachikwa jina la Yuda Msaliti au Yuda Iskariote kutokana na kuonesha usaliti kwa wapenzi wa kaka yake. Anafananishwa na yule Yuda aliyemsaliti Yesu, akasulubiwa na kufa msalabani.

Esma ambaye alikuwa mke wa ndoa wa meneja wa wasanii wa Bongo Fleva, Hamad Manungwi ‘Petit Man’ kabla ya kutengana na kurudiana kisha kuachana tena na sasa wamerudiana.

Kwenye mahojiano maalum (exclusive interview) ya ana kwa ana na  gazeti moja la kila wiki Esma ambaye pia ni mwanamama mjasiriamali, anafunguka mambo mengi yaliyotokea kwenye ndoa yake na mfanyabiashara Yahaya Msizwa ambayo ilidumu kwa miezi mitatu tu;

MWANDISHI: Mambo vipi Esma?

ESMA: Salama, leta habari maana ninyi huwa hamna dogo…

MWANDISHI: Sisi tupo sawa kabisa, tunataka mapya kutoka kwako.

ESMA: Haya nipo tayari, ninayajua maswali yenu…

MWANDISHI: Ulikuwa kimya sana baada tu ya kufunga ndoa na Msizwa kwani hata kwenye mitandao ulijiondoa kabisa, ni mume alitaka hivyo?

ESMA: Hapana, niliamua mwenyewe kutuliza akili yangu; yaani hata kwenye mitandao sikuonekana kabisa. Niliamua kwanza niwaumize vichwa walimwengu.

MWANDISHI: Watu walidhani mumeo alikuzuia kuingia mitandaoni…

ESMA: Asingeweza kunizuia kwa sababu alinikuta hivyo, isipokuwa niliamua tu kuwa hivyo.

MWANDISHI: Vipi kuhusu biashara maana watu walikuwa wakifika dukani kwako, Afrika Sana (Sinza jijini Dar) hawakuoni…

ESMA: Nilipumzika kwa muda wa miezi minne, nikaamua kuwaachia wasichana wangu waendelee na kazi za dukani.

MWANDISHI: Kwenye mitandao zilizagaa picha ukiwa hoi unaumwa, ni nini hasa kilikuwa kinakusumbua?

ESMA: Niliishiwa tu na damu, lakini sikuwa na shida yoyote.

MWANDISHI:Mbona kulikuwa na madai kuhusiana na kutoa ujauzito wa mumeo na mpaka akaweka mshumaa kwenye ukurasa wake wa Instagram

ESMA:Itakuwa labda alikumbuka vitu vingine, lakini mimi sijawahi kutoa mimba.

MWANDISHI: Baadhi ya watu walidhani ulipokuwa ukisema mambo ya Mama Melo labda ni utani, kumbe ni kweli ni mke mwenzako?

ESMA: Ni kweli kwani hata nilipoolewa si nilikuwa ninajua ninaolewa mke tatu?

MWANDISHI: Sasa vipi kuhusu madai ya kuachana au bado uko kwenye ndoa yako?

ESMA: Hapana! Kwa sasa nipo singo.

MWANDISHI: Lakini ndoa yako itakuwa imeweka rekodi ya kudumu kwa miezi mitatu tu kisha ikavunjika…

ESMA: Ukiwa mkweli na huru utaishi maisha mazuri, watakaofikiria nimeweka rekodi basi sawa.IJUMAA: Kuna madai kwamba umerudiana na mtalaka wako Petit Man, vipi kuhusu hilo?

ESMA: Ila watu wana vituko sana, wanashindwa kutambua kuwa yule ni baba wa mtoto wangu, walitaka hata nisisalimiane naye?

MWANDISHI: Kwenye msiba wa mama yake Petit Man mlionekana karibu familia nzima mmekwenda msibani, sasa kwa upande wa mumeo wanasema juu ya hilo?

ESMA: Upande upi tena? Hata kama tumeenda, tuna haki kwa sababu ni bibi wa mwanangu na alikuwa rafiki yangu sana.

MWANDISHI: Kwenye msiba, Petit hakuweza kuficha hisia maana kila mara alikuwa anakufuata, ulikuwa unapata picha gani?

ESMA: Umesahau kuwa penzi la kweli halifi? Litakuwepo tu hata kama mtu anaoa au anaolewa.

MWANDISHI: Hivi karibuni alikuja wifi yako wa zamani, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady ’ na watoto, lakini sikukuona umekwenda kumpokea au kupiga naye picha japo ulionekana kufurahi sana ujio wake, ni kwa nini?

ESMA: Ni kwa sababu nilikuwa kwenye harakati zangu, lakini tuliwasiliana.

MWANDISHI: Alipokuja Zari hukutamani aendelee kukaa moja kwa moja kama wifi yako?

ESMA: Zari ni mama wa watoto wetu na kuhusu kuwa wifi, hilo ni jukumu la Diamond mweyewe.

MWANDISHI: Uliweka wazi kuwa gari ulilozawadiwa halikuwa la kweli, ni nini kilitokea?

ESMA: Sijajua, lakini kweli halikuwa langu maana lilirudi lilipotoka na ninachoshukuru nina gari langu.

MWANDISHI: Kwenye mtandao niliona ulimuweka wazi baba wa mtoto wako wa kwanza, ulifikiria nini?

ESMA: Ni kwa sababu ni baba yake na niliamua kuweka wazi na hata mwanangu ajisikie vizuri.

MWANDISHI: Kwa hiyo bado unakaa kwenye nyumba aliyokupangia mumeo?

ESMA: (kicheko) hilo siwezi kulijibu kwa sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here