Na Mwandishi Wetu
MSANII Abdulaziz Chande maarufu Dogo Janja amefunguka kuwa mipago ya ndoa yake imekalimika kwa asilimia kubwa.
Dogo Janja ambaye alimvisha pete ya uchumba wake Queen Linah miezi michache iliyopita alisema, kwa sasa mambo yanaendelea baina ya pande mbili za familia na wakati wowote yanaweza kukamilika.
“Tupo kwenye hatua nzuri ya mipango yetu ya kumaliza safari ya maisha yetu, kufunga ndoa, nje watu hawajui kinachoendelea lakini niwaambie tu mipango imekamilika kwa asilimia 95, kilichobaki ni padogo sana”alisema Dogo Janja.
Kuhusu kuwa mbali anakoishi mtarajiwa wake mjini Arusha nay eye akiishi Dar, Dogo Janja alisema hapati tatizo lolote la yeye kuwa mbali na mpenzi wake.