Dk. Mwinyi atengua uteuzi wa katibu wa Rais

0

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa katibu wa rais, Suleiman Ahmed Saleh ikiwa umepita mwezi mmoja tangu alipomteua ikielezwa kuwa sasa atapangiwa kazi nyingine.

Dk Mwinyi alimwapisha Ahmed Novemba 7, 2020 katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Unguja.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Desemba 14, 2020 na katibu mkuu kiongozi, Dk Abdulhamid Mzee  inaeleza kuwa rais Mwinyi amechukua hatua hiyo kutokana na uwezo alionao kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.

“Chini ya kifungu cha Na.53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12(3) cha Sheria ya Utumishi wa umma Namba 2 ya mwaka 2011, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa katibu wa Rais, Suleiman Ahmed Saleh,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ikibainisha kuwa atapangia kwazi nyingine.

Taarifa hiyo haikueleza sababu ya Rais Mwinyi kutengua uteuzi huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here