Dk. Gwajima Wizara ya Afya iwe ya mfano kiutendaji, utoaji huduma kwa wananchi

0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima amewataka viongozi na watumishi wa  hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia mabadiliko ya teknolojia ili kuongeza tija ili kuifanya kuwa Wizara ya mfano kiutendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dk. Gwajima ameyasema hayo leo Desemba 10, jijini Dodoma alipowasili Ofisni kwake kwa mara ya kwanza baada ya kiapo na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Wizara hiyo na kutoa mwelekeo wa utendaji kazi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akitoa mwelekeo wa Utendaji, Waziri Dk. Gwajima amesema wizara hiyo inatakiwa kuwa Wizara ya Mfano katika uongozi na kuongeza chachu katika mafanikio yaliyopatikana ikilenga utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

“Tunataka kuongeza vikorombwezo vikatavyojibu hotuba ya Rais wakati akizindua Bunge la kumi na mbili, kujibu na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa kasi kubwa na kutekeleza ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ” alisisitiza Dk. Gwajima.

Ameongeza kuwa umefika wakati kwa watumishi wa Wizara ya Afya kupata majawabu ya changamoto kwa kutumia mfumo wa kisasa ili kupunguza muda wa ufuatiliaji na kuharakisha utoaji wa huduma.

Amewataka watumishi kushikamana na kuondokana na matabaka yanayoweza kusababisha mgawanyiko na hatimaye kukwamisha utendaji kazi wa Wizara na taifa kwa ujumla wake

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here