
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk. Leonard Chamuriho amewataka watumishi wa wizara Ujenzi na Uchukuzi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi ili kuongeza ufanisi.
Akizungumza na menejimenti ya Sekta ya Ujenzi na Uchukuzi mara baada ya kuwasili ofisini hapo jijini Dodoma ameitaka menejimneti kuunganisha wafanyakazi wa sekta zote kufanya kazi kwa kuzingatia matokeo yanayopimika.
“Jipangeni kuhakikisha kuwa Watumishi wote wanafanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kufikia malengo yanayotarajiwa na Serikali katika kuboresha miundombinu nchini’ amesema Chamuriho.
Amemtaka Katibu Mkuu-Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga na Kaimu Katibu Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire kuhakikisha miradi yote inayoendelea ujenzi wake unakamilika kwa wakati na tija.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, mhandisi Godfrey Kasekenya ameitaka menejimenti ya Wizara kuweka ratiba ya mara kwa mara ya kukagua miradi ili kupata taarifa ya maendeleo na kuchukua hatua mapema kwa miradi yenye changamoto.
Akiwakaribisha Waziri na Naibu Waziri, Katibu Mkuu Ujenzi amewahakikishia viongozi hao ushirikiano kati yao menejimenti na watumishi kwa sekta anazosimamia.
Waziri Chamuriho na Naibu Waziri Eng. Godfrey Kasekenya walikuwa katika kikao cha kwanza cha na menejimenti ya wizara mara baada ya kuteueliwa kuongoza wizara hiyo hivi karibuni.

Pamoja na menejimenti ya Wizara hiyo, mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za
Wizara hiyo, jijini Dodoma.