Home BURUDANI Diamond Platnumz afikishwa mahakamani

Diamond Platnumz afikishwa mahakamani

NA MWANDISHI WETU

Nyota wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Naseeb Juma maarafu kwa jina Diamond Platnumz, ameshitakiwa katika Mahakama ya Ardhi ya Mwananyamala Dar es Salaam, akishtakiwa kwa uharibifu wa mali zenye thamani ya shilingi milioni 337 katika nyumba aliyokuwa amepanga kwa matumizi ya Studio eneo Sinza Morri, kabla ya kuhamia Mbezi.

Mmiliki wa nyumba hiyo, Maulidi Wandwe amesema fedha hizo ni pamoja na kodi ya mwaka mmoja ambayo mwanamuziki huyo hakuilipa.

Naye Wakili wa Diamond amesema mteja wake yuko nje ya nchi na atachelewa kurejea nchini kutokana tishio la maambukizi ya virusi vya Corona.

Aidha kesi hiyo itaendelea tena kesho Machi 18.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular

Yanga yampatia Tshishimbi mkataba mpya

NA MWANDISHI WETU Klabu ya Yanga SC, imesema kuwa tayari imemaliza kazi yake ya kuhakikisha inambakiza kiungo tegemeo wa...

Tetesi za soka barani Ulaya

SANCHO AITIKISA UNITED Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jadon Sancho (20), amesema hatakuwa tayari...

Makonda: Wazururaji hawatakwenda mahabusu watazibua mitaro ya maji machafu

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa watu watakaokamatwa kwenye mkoa huo kutokana...

Chui katika hifadhi ya wanyama ya Bronx akutwa na Virusi vya Corona

NEW YORK, MAREKANI Chui wa kike wa Malaysia aliyefahamika kwa jina la Nadia mwenye umri wa miaka minne katika hifadhi...

Recent Comments