DC Kinondoni atangaza operesheni kwa wanaopandisha bei ya saruji

0

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo ametangaza Operesheni kali dhidi ya wauza Saruji kwa bei ya Rejareja ambao wamepandisha bei kutoka Sh 14, 000 au 15, 000 14 hadi 20, 000 kwa mfuko mmoja wa Saruji kwa kisingizio cha kuwepo uhaba wa bidhaa hiyo kutoka Viwandani.

DC Chongolo ameagiza kufanyika kwa ukaguzi wa duka kwa duka baada ya kubaini kuwa wafanyabiashara hao wamekiuka bei elekezi, baada ya kujiridhisha kwamba kuna Saruji ya kutosha inayozalishwa katika kiwanda cha Wazo wakati alipotembelea kiwanda hicho mapema leo.

Amesema kiwanda cha Wazo kinazalisha tani elfu sita kwa siku na hakuna uhaba wa Saruji au kuongezeka kwa bei ya bidhaa hiyo kwa mfuko mmoja kama inavyoelezwa na baadhi wauzaji wa saruji kwa bei ya rejareja.

Meneja Biashara wa kiwanda cha twiga cement cha wazo Mhandisi Danford Semwenda amesema Pamoja na kuwapo kwa Mahitaji makubwa ya Saruji yanayotokana na Miradi mbali mbali mikubwa inayoendelea katika jiji la dsm bado uzalishaji wa Saruji unaendelea kama kawaida na bei ya kiwandani haijapanda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here